Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

08 NOVEMBA 2022

08 NOVEMBA 2022

Pakua

Hii leo katika Habari za UN tunakuletea Habari kwa Ufupi, Mada kwa Kina na Mashinani na zote zikiwa ne mrengo wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi unaofanyika huko Sharm el-Sheikh nchini Misri.

  1. Habari kwa Ufupi: Ripoti ya UNICEF kuhusu mafuriko kuathiri watoto milioni 27.7 duniani kote; WMO kutaka viongozi wachukue hatua kuhusu namna ya kutumia vema maji kama suluhu ya mabadiliko ya tabianchi; Mwandishi mshirika wetu Joyce Shebe akiwa Sharm el-Sheikh anatupatia kile kilichosemwa na marais wa Tanzania, Malawi na Kenya.
  2. Mada kwa kina: Flora Nducha akiwa Kigali nchini Rwanda ametembelea mradi wa vijana Greencare Liimted wakihakikisha wanadhibiti utupaji taka kama njia ya kulinda mazingira.
  3. Mashinani: Mwanaharakati kijana Leah Namugerwa kutoka Uganda akiwa huko Sharm el-Sheikh anahoji iwapo viongozi wanataka wakumbukwe kama walikuwa madarakani bila kufanya lolote au vipi?

Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.

Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
10'38"