Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

21 NOVEMBA 2022

21 NOVEMBA 2022

Pakua

Hii leo jarida linaangazia siku ya uvuvi, masuala ya watoto na makala tunakwenda nchini Somalia kumulika uhakika wa chakula kwa watu waliokumbwa na changamoto ya ukame na mafuriko, mashinani ni ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

  1. Ikiwa leo ni siku ya uvuvi duniani imeelezwa kuwa sekta ya uvuvi ni muhimu sana katika kuhakikisha uhakika wa chakula na inasaidia mtu 1 kati ya 10 duniani kote. Kwa kutambua mchango wake wito umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO kuboresha maisha ya mamilioni ya wanawake kwa wanaume wanaofanyakazi katika sekta hii kwa kuhakikisha haki zao za binadamu zinatimizwa.
  2. Nchini Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto UNICEF kwakushirikiana na wadau wake wameanzisha mradi wakujenga vyoo uitwao Fresh Life lengo ni kusaidia kuhakikisha wananchi wanapata ufikiaji wa vyoo safi, salama pamoja na usafi wa mazingira na matokeo yake ni kupunguza ugonjwa wa Kipindipindu kwa kiingereza Cholera.
  3. Makala inamulika hatua za Umoja wa Mataifa za kuwezesha wananchi waliokumbwa na ukame kuendelea kupata kipato na wakati huo huo kuwa na uhakika wa chakula, kulikoni?
  4. Na leo mashinani tunasikia sehemu ya ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa baada ya Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa Mkataba wa mabadiliko ya tabianchi COP27

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
12'29"