Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

17 NOVEMBA 2022

17 NOVEMBA 2022

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia mada kwa kina na leo tunafunga safari hadi bara Hindi huko nchini India kusikia kuhusu kijiji cha kwanza nchini humo kinachotumia nishati ya sola pekee kwa wakazi wake zaidi ya 6,400.  Pia litakuletea Habari kwa ufupi kama zifuatayo:

  1. Ikiwa ni miaka miwili tangu kuzindiliwa mkakati wa kimataifa wa kusongesha hatua za kutokomeza saratani ya shingo ya kizazi na kuweka taarifa za hatari ya kupata saratani hiyo kwa wanawake wanaoishi na virusi vya ukimwi VVU , shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO linasema kuna hatua zilizopigwa katika nyanja zote. 
  2. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amekaribisha makubaliano yaliyofikiwa na pende zote ya kuendelea na mpango wa usafirishaji nafaka wa bahari Nyeusi bila bughdha ili kuwezesha kusafirisha nafaka, vyakula vingine na mbolea kutoka Ukraine. 
  3. Na shirikisho la soka duniani FIFA na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO kwa kushirikiana na wizara ya afya ya Qatar na kamati kuu ya uwasilishaji na historia  SC leo wamezindua kampeni ya #BringTheMoves challenge, ikiwachagiza wasakata kabumbu kwenye mashindano ya kombe la dunia la mwaka huu linaloanza jumapili Novemba 20 kutimiza changamoto waliyopewa kwenye mitandao ya kijamii  na mashabiki wao ya kuwachagiza Watoto na vijana kufanya mazoezi.

Kisha ni kujifunza lugha ya Kiswahili na tunakwenda Zanzibar nchini Tanzania kwake Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar, BAKIZA. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
12'23"