Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

29 DESEMBA 2023

Miongoni mwa yaliyomo kwenye Jarida la Habar iza UN:

Kikosi cha kwanza cha SADC chawasili DRC.

ILO yanusuru wanawake na mfumo wa utumwa nchini Niger.

Makala leo tunakwenda Kenya kumulika jinsi mfumo wa fedha wa kuwezesha wakulima kukabiliana na kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi.

Na mashinani na fursa ni yake Agnes Abisa, Afisa Habari na Mawasiliano wa YUNA ambayo ni Jumuiya ya Vijana ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.

Sauti
9'59"

28 DESEMBA 2023

Hujambo na karibu kusikiliza jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili  ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni Alhamisi ya tarehe 28  ya  mwezi Desemba takribani siku 4 panapo majaliwa kuumaliza mwaka huu wa 2023. Mimi ni ASSUMPTA MASSOI ninakukaribisha kusikiliza mkusanyiko wa matukio machache kati ya mengi yaliyojiri katika mwaka huu ambapo Umoja wa Mataifa ulikuwa na jukumu zito kuhakikisha pamoja na yote bado dunia inasalia kuwa mahali salama pa kuishi. 

Sauti
14'9"