Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

14 NOVEMBA 2022

14 NOVEMBA 2022

Pakua

Hii leo katika Habari za UN mwenyeji wako akiwa Assumpta Massoi tunamulika ugonjwa wa kisukari barani Afrika, jawabu la nishati salama Malawi, vijana na wito wao huko Sharm el- sHeikh kwenye COP27 na ujumbe wa Balozi mwema wa IFAD Sabrina Dhowre Elba.

1. Wakati dunia ikiadhimisha hii leo siku ya kisukari duniani kwa lengo la kuelimisha umma kuhusu ongezeko la mzigo wa ugonjwa huo na mikakati ya kuzuia na kudhibiti tishio lake, bara la Afrika linaonekana kuwa na changamoto kubwa ya ugonjwa huo, kwa mujibu wa takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO

2. Nchini Malawi, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, UNDP limewezesha serikali kutumia mito na jua kama vyanzo vya nishati na hivyo kusaidia zaidi ya kaya 3,000 kupata nishati salama na nafuu na sasa hata vipato vyao vimeongezeka halikadhalika kuepusha vifo vya wajawazito.

3. Makala: Tunakwenda nchini Misri katika mji wa Sharm el-Sheikh ambako  vijana kutoka kila kona ya dunia wamekusanyika kuhudhuria mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP27 na wanataka kuhakikisha kwamba uwepo wao si tu unaonekana bali ujumbe waliopeleka unasikika na hatimaye uweze kufanyiwa kazi.

4. Mashinani: Balozi mwema wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo IFAD Sabrina Dhowre Elba ametoa wito kwa mataifa tajiri duniani kuhakikisha yanasaidia wakulima wadogo vijijini.

Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
13'4"