Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

30 DESEMBA 2022

Jaridani leo Ijumaa ya tarehe 30 mwezi Desemba mwaka 2022 tunakuletea habari za maombolezo na pia ya uteuzi wa naibu mkurugenzi mtendaji mpya wa UNEP.  Makala tunaelekea nchini Kenya katika makazi ya wakimbizi ya Kalobeyei na mashinani tunaangazia haki za wanawake na wasichana Afghanistan.

Sauti
11'6"

29 DESEMBA 2022

Hii leo tunakuletea jarida maalum likimulika kwa muhtasari yaliyojiri mwaka huu na matarajio kwa mwaka 2023 na pia habari kwa ufupi zikiwemo heri ya mwaka mpya kutoka katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, hali ya usalama katika Greater Jonglei nchini Sudan Kusini na wanawake na wasichana kukatazwa kufanya kazi na mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs. nchini Afghanistan.

Sauti
13'58"

28 DESEMBA 2022

Hii leo jaridani tunakuletea habazi za UNCTAD na kazi za Umoja wa Mataifa nchini CAR. Makala tunakupeleka Karamoja nchini Uganda na mashinani tunakuletea ujumbe wa WFP kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

Sauti
9'58"

27 Desemba 2022

Hii leo katika jarida la Umoja wa Mataifa utasikia mada kwa kina kuhusu utalii endelevu nakulinda wanyamapori walio hatarini kutoweka nchini Tanzania.

pia utasikia habari kwa ufupi kuhusu marufuku ya wanawake nchini Afghanistan kufanya kazi kwenye NGOs, Wakimbizi waliokwama baharini kwa mwezi mzima waokolewa na Indonesia na Wakimbizi wa ndani nchini Ukraine wapatiwa msaada katika msimu huu wa baridi. 

Na tukiwa bado kwenye msimu wa sikukuu, wakimbizi kutoka nchini Ukriane wanajaribu kufanya kila jitihada kuhakikisha nao wanasherehekea sikukuu hizi.

Sauti
13'5"

23 DESEMBA 2022

Jaridani leo Ijumaa ya tarehe 23 ya mwezi Desemba mwaka 2022 tnakuletea habari za WHO na habari kuhusu machafuko jimboni Upper Nile nchini Sudan kusini.  Makala tunakwenda nchini CAR na mashinani nchini Kenya.

Sauti
11'14"

22 DESEMBA 2022

Ni Alhamisi ya tarehe 22 mwezi Desemba mwaka 2022 ambapo leo ni kipindi maalumu kwa ajili ya shukrani kwako msikilizaji wetu na pia kutakiana salamu za Christmas. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo kutoka nchini Afghanistan, Sudani Kusini na Myanmar.

Sauti
12'41"

21 DESEMBA 2022

Hii leo jaridani tunamulika haki za wasichana na wanawake nchini Afghanistan na mkopo wa IMF nhini Kenya. Makala tunakupeleka nchini Zambia na mashinani tunakwenda nchini Mali kumulika UNICEF na harakati za kunasua watoto walioathirika na majanga yanayokumba taifa hilo.

Sauti
12'7"

20 DESEMBA 2022

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo tunakupeleka nchini Tanzania kusikiliza simulizi ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye baada ya kukimbia machafuko nchini mwake sasa ana hadhi ya uhamiaji nchini Tanzania. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo njaa Somalia, hatari za majanga, na madhara ya mazingira Iran. Mashinani tutaelekea nchini Msumbiji ambako tutashuhudia kuwa jamii ikiamua, hakuna mwanajamii atakayeachwa nyuma.

Sauti
11'38"

19 DESEMBA 2022

Hii leo jaridani tunakuletea habari kutoka mkutano wa COP 15, na nchini Tanzania, makala tunasalia nchini humo mkoani Morogoro na mashinani tunakuletea ujumbe kuhusu bayoanuai. 1. Ikiwa leo ni tamati ya mkutano wa 15 wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa kuhusu bayonuai, COP15, huko Montréal, Canada, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, limekaribisha makubaliano ya kihistoria yaliyofikiwa katika mkutano huo kuhusu mpango mpya wa kuhifadhi na kulinda asili kwa kutumia Mfumo mpya wa Kimataifa wa Bayonuai, (GBF).
Sauti
14'39"

16 DESEMBA 2022

Jaridani leo Ijumaa ya tarehe 16  ya mwezi Desemba mwaka 2022 tunakuletea habari kuhusu uhamiaji na kazi za walinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC.  

Sauti
11'31"