Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

31 DESEMBA 2020

Katika Jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Anold Kayanda anakuletea salamu za mwisho wa mwaka kutoka kwa wafanyakazi

-Wanazungumzia mambo mbalimbali ikiwemo malengo ya maendeleo endelevu SDGs

-Je mwaka 2020 umekuwaje?

-Nini changamoto kubwa iliyokabili kazi zao kwa mwaka 2020

-Mashinani washirika wetu na maripota wetu wanasemaje?

-Na nini msikilizaji, mtazamaji, na mfuatiliaji wa vipindi vya Umoja wa Mataifa atarajie mwaka 2021

 

Sauti
9'57"

30 DESEMBA 2020

Katika Jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea matukio ya mwaka 2020

-Mwaka 2020 ulitangazwa kuwa mwaka wa wauguzi na wakunga na shirika la afya duniani WHO

-Janga la corona au COVID-19  Machi mwaka huu lilitangazwa kuwa janga la kimataifa. Na kwa mujibu wa WHO nchi 222 duniani zimeathirika huku watu zaidi ya milioni 1 na laki 7 wakipoteza maisha na wengine zaidi ya milioni 79 wameambukizwa ugonjwa huo

Sauti
11'45"

29 DESEMBA 2020

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Kenya limetoa msaada wa Redio 10,000 zinazotumia nishati ya jua au sola ili kuwawezesha watoto wengi kutoka kaya masikini kusomea nyumbani wakisubiri kurejea shuleni

-Maefu ya watu waliokimbia mapigano Tigray Ethiopia wamepitia madhila mengi lakini kina mama wajawazito ni zaidi, leo utamsikia mmoja wa wakimbizi hao aliyelazimika kujifungulia ugenini.

Sauti
12'22"

28 DESEMBA 2020

Karika jarida la mada kwa kina hii leo Flora Nducha anakuletea

- Mashirika ya Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na la mpango wa chakula WFP kwa kushirikiana na serikali ya Ethiopia wamewafikishia msaada wa chakula wakimbizi 25,000 kutoka Eritrea walio katika kambi za wakimbizi jimboni Tigray

-Mpango wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika wa kulinda amani Darfur Sudan UNAMID umetoa mafunzo ya huduma ya kwanza, ushonaji barakoa na kutengeneza sabuni kwa wanawake wafungwa 30 mjini El Fasher

Sauti
12'9"

24 DESEMBA 2020

Katika Jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA linasema mwaka 2020 ulikuwa mwaka wa zahma kubwa kwa wanawake na wasichana, utamsikia mkurugenzi mtendaji Dkt. Natalia Kanem akiuelezea

-Wakulima nchini Senegal wanufaika na mradi wa PAFA unaofadhiliwa na shirika la kimataifa la maendeleo ya kilimo IFAD

-Huko nchini Togo shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO lakidhi kiu ya ya wakazi wa danpen kwa kukarabati bwawa kwa ajili ya umwagiliaji, kulisha mifugo na utalii

Sauti
11'15"

23 Desemba 2020

UNICEF yaingilia kati kuokoa watoto Korogocho Kenya. 


Mradi wa maji Malawi waondoa adha kwa wanafunzi kuchelewa darasani.


Na wapiga kura nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, wameanza kuchukua kadi zao za mpiga kura tayari kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika jumapili hii ya tarehe 27 mwezi Desemba.
 

Sauti
12'16"

22 DESEMBA 2020

Leo mwenyeji wako ni Anold Kayanda anaanzia huko Cabod Delgado nchini Msumbiji kisha Lebanon kwa wakimbizi wa Syria na halafu nchini Sudan Kusini kuangazia umuhimu wa radio katika kuelimisha umma. Makala tuko Tanzania na mashinani tunamleta kwako Angelina Jolie. Karibu!

Sauti
12'37"

21 DESEMBA 2020

Hii leo jaridani ni mada kwa kina na tunakwenda mkoani Mwanza nchini Tanzania ambako shirika la Amani girls home wameanzisha mradi unaowawezesha wasichana hususani wale waliokumbwa na changamoto mbalimbali za kimaisha, ili waweze kufikia malengo yao kwa kuwapa ujuzi mbalimbali. Lakini tuna Habari kwa Ufupi ikimulika Burkina Faso, Mali na kubabuka kwa matumbawe Mashinani tunabisha hodi DRC. Karibu na mwenyeji wako ni Anold Kayanda.

Sauti
11'25"

18 Desemba 2020

Ikiwa leo ni siku ya wahamiaji duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema ni mwaka wa kutathmini jinsi janga la Corona au COVID-19 lilivyosababisha mamilioni ya watu kukumbwa na machungu ya kutengana na familia zao na kutokuwa na uhakika wa ajira, jambo ambalo limewapatia watu hisia halisi ambazo wahamiaji hukumbana nazo kila wakati kwenye maisha yao. 

Sauti
11'28"