Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

10 NOVEMBA 2022

10 NOVEMBA 2022

Pakua

Katika Jarida la habari la Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea 

-Huko Sharm el Sheikh kwenye mkutno wa COP27 vijana watoa wito kwa nchi wachafuzi wa mazingira kugharamia hasara na uharibifu wa janga hilo

-Nchini Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO washikana na jeshi la serikali FARDC kuendesha doria kulinda raia

-Nchini Lebanon shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na wadau wa chanjo wafikisha chanjo 600,000 kwa ajili ya kampeni dhidi ya kipindupindu itakayoanza Jumamosi

-Mada yetu kwa kina inatupeleka COP27 Sharm el Sheikh Misri ambapo leo utasikia sauti mbalimbali kutoka kwa viongozi wa kisiasa, jamii za asili na vijana

-Na katika kujifunza Kiswahili tunabisha hodi Tanzania Baraza la Kiswahili la Taifa BAKITA kupata ufafanuzi wa neno MUKU

Audio Credit
UN News/Assumpta Massoi
Audio Duration
13'40"