31 DESEMBA 2021
Katika jarida la matukio ya mwaka la Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea
-Wanajeshi watatu wa kulinda amani kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA, wamejeruhiwa na mmoja vibaya sana baada ya msafara wao kukanyaga vilipuzi. Wote wanatibiwa hospitalini mjini Bangui
-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema mwaka huu umekuwa wa machungu na ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto katika mizozo ya muda mrefu na ile mipya.