Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

11 NOVEMBA 2022

11 NOVEMBA 2022

Pakua

Hii leo katika Habari za UN tunamulika msaada wa kibinadamu, tabianchi, mafuriko Nigeria na hakarati za kukabili mmomonyoko wa udongo Kenya.

  1. Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP linasema iwapo halitapokea fedha za nyongeza, litalazimika kusitisha msaada muhimu wa kibinadamu kwa wakazi milioni moja wa jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji ifikapo kilele cha msimu wa njaa mwezi Februari mwakani kutokana na ukata unaokabili.
  2. Mkurugenzi wa masuala ya utafiti na matumizi ya hali ya hewa kutoka Mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania TMA Dr. Ladislaus Chang'a amesema ni vyema wataalamu wa Afrika wakaongeza kasi katika kufanya tafiti na kuzichapisha katika majarida ya kimataifa ili tafiti zao ziweze kutumika katika utungaji wa será za kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

  3. Makala inatupeleka Nigeria ambako mabadiliko ya tabianchi yamesbabisha mafuriko makubwa yaliyoambatana na athari mbaya ikiwemo vifo, kubomoa nyumba na kusambaratisha mioundombinu mingine muhimu katika jamii.

  4. Mashinani nampisha Jackson Lakaya, mfugaji kutoka kijiji cha Saswa kaunti ya Narok nchini Kenya akielezea ni kwa vipi mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo, UNDP limewawezesha kukabiliana na mmomonyoko wa udongo.

Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
12'11"