Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

16 Novemba 2022

16 Novemba 2022

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia mabadiliko ya tabianchi na athari kwa wakimbizi, ziara ya afisa wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Makala tunamulika haki za wenye ualbino Uganda na mashinani tunamulika nafasi ya wananawake kwenye maamuzi.

1. Endapo uwekezaji wa haraka hautofanyika katika njia za kupambana na mabadiliko ya tabianchi na kujenga mnepo katika nchi za Sahael , basi kuna hatari ya kuwa na miongo ya vita vya silaha na watu kuendelea kutawanywa vinavyochochewa na ongezeko la joto duniani , uhaba wa rasilimali na kutokuwa na uhakika wa chakula limeonya leo shirika la Umoja wa Mastaifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa kushirikiana na mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya maendeleo.

2. Wakati idadi ya wakimbizi wa ndani nchini Sudan ikizidi kuongezeka ambapo mpaka sasa wamefikia milioni 3.7 na kati yao 200,000 wakiwa wamerekodiwa mwaka huu pekee Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amefunga safari mpaka nchi huko kwenda kuzungumza na wawakilishi wa wakimbizi, asasi za kiraia na serikali.

3. Makala na tunakwenda nchini Uganda ambako huko ndoto ya mtoto mmoja mwenye ualbino ya kutaka kuwa rubani almanusura itumbukie nyongo, lakini harakati za serikali ya Uganda na Umoja wa Mataifa zimeirejesha ndoto hiyo, kulikoni?

4. Mashinani wakati mkutano wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi COP27 ukiendelea nchini Misri, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed anasema wanawake na wasichana ni viongozi muhimu na Madhubuti wa kushughulikia changamoto za mabadiliko ya tabianchi lakini hawathaminiwi na wanapuuzwa.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Duration
13'28"