Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UNTV

Mashambulizi na umwagaji damu vinaendelea Gaza licha ya kuanza kwa Ramadhan mauaji - Guterres

Leo ni mwanzo wa mwezi mktukufu wa Ramadhan ambapo Waislamu kote duniani husherehekea na kuchagiza tunu za amani, maridhiano na mshikamano lakini uhasama unaendelea hususani sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Gaza ambako mauaji , na mashambulizi hayajakoma amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani hii leo. 

Sauti
2'53"
© CIAT/Neil Palmer

IFAD: Mradi wa ukulima nchini Malawi waboresha maisha ya na usawa kijinsia katika jamii

Nchini Malawi Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya Kilimo IFAD unatekeleza mradi wa kuwasaidia wanawake wa vijijini kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia na sasa wananachi wanafaidi matunda yake. 

Mradi huo uitwao TRADE ulioanzishwa mwaka 2022 na serikali ya Malawi kwa kushirikiana na IFAD inalenga kubadilisha kilimo kupitia mpango wake wa Mseto na Ujasiriamali. 

Sauti
2'18"
Picha kwa hisani ya Zulaikha Patel

Ukatili dhidi ya wanawake Afrika kusini: Polisi 'wanolewa' sasa mambo ni shwari

Nchini Afrika Kusini katika jimbo la Western Cape kufuatia mafunzo kuhusu unyanyasaji wa kijinsia yaliyotolewa na kikundi cha wanawake cha Ilitha Labantu kwa vituo kadhaa vya polisi, sasa kuna ushahidi wa wazi kwamba vituo vya polisi vimeweka mazingira rafiki ya kuwasikiliza wanawake walionyanyaswa kuliko ilivyokuwa hapo awali. Anold Kayanda ameufuatilia mradi huo. Karibu Anold utueleze zaidi.

(Taarifa ya Anold Kayanda)

Sauti
1'54"
©TANZBATT 9 / Private Sosper Msafiri

Mtoto Charles: MONUSCO imenitoa msituni, asanteni sana

Harakati za ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, za kuondoka nchini humo zikiendelea, tunamulika hatua chanya zilizochukuliwa na ujumbe huo katika kunusuru vijana waliokuwa wanatumikishwa na waasi mashariki mwa nchi hiyo.

Miongoni mwao ni Charles, mwenye umri wa miaka 16 ambaye si jina lake halisi. Yeye alitumikishwa msituni na waasi kwa kipindi cha miaka miwili.

Audio Duration
2'19"
© WFP/Hugh Rutherford

WFP/UNICEF: Janga kubwa la njaa duniani linanyemelea Sudan miezi 11 baada ya kuzuka vita

Takriban miezi 11 tangu majenerali wapinzani watangaze vita nchini Sudan, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa leo walionya kwamba mzozo huo unaweza kusababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani. 

Sudan, nchi iliyo kaskazini mashariki mwa Afrika tayari iko katika mzozo mkubwa zaidi wa watu waliofuriushwa makwao duniani kwa mujibu, Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa, WFP.

Sauti
2'32"
© UNRWA/Ashraf Amra

UN inaonya kwamba vita ya Gaza yaweza kuchochea machafuko zaidi ya kikanda

Mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza yanaendelea nchini Misri kwa siku ya pili leo huku Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa akionya kwamba vita ya Gaza iko katika hatari ya kubadili mweleko na kupanua wigo zaidi utakaoathiri kila nchi Mashariki ya Kati na kwingineko. 

Asante Anold. Kamishina Mkuu Volker Türk ameliambia Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswisi kuwa "Nina wasiwasi mkubwa kwamba katika janga hili la vita cheche yoyote zaidi inaweza kusababisha moto mkubwa zaidi," 

Sauti
1'41"
© UN Photo/Isaac Billy

UNMISS: Kuondoa mabomu ya ardhini Sudan Kusini eneo sawa na viwanja 64 vya soka limesafishwa

Nchini Sudan Kusini kwa mwaka jana pekee wateguaji wa mabomu ya ardhini wa Umoja wa Mataifa wamefanikiwa kusafisha eneo lenye ukubwa sawa na viwanja 64 vya mpira wa miguu, na hivyo kuondoa hatari nyingi za milipuko, inaeleza UNMISS ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini.

Kupitia Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya misaada ya kutegua mabomu yaliyotegwa ardhini (UNMAS) asilimia 70 ya vilipuzi ambavyo vilikuwa havijalipuka sasa vimeharibiwa au kuondolewa katika maeneo vilimokuwa na hivyo kuwahakikishia watu makazi salama na maeneo ya kilimo.

Sauti
1'6"
Unsplash/Christopher William

Mtu 1 kati ya 4 anaishi na utipwatipwa duniani

Utafiti mpya uliotolewa leo na jarida la kitabibu la Uingereza Lancet na shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO unaonyesha kwamba, mwaka 2022, zaidi ya watu bilioni 1 duniani sasa wanaishi na unene wa kupindukia ama utipwa tipwa. Duniani kote, unene wa kupindukia kwa watu wazima umeongezeka zaidi ya mara mbili tangu mwaka 1990, na umepanda mara nne kwa watoto na vijana wenye umri wa miaka 5 hadi 19. 

Sauti
2'48"
UN Photo/Evan Schneider (Maktaba)

Guterres: Umoja wa Mataifa hauondoki Sudan

Ikiwa leo ndio siku ya mwisho ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia kipindi cha mpito nchini Sudan (UNITAMS), Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema pamoja na kwamba UNITAMS inaondoka Sudan lakini Umoja wa Mataifa hauondoki nchini humo na unaendelea kujitolea kwa dhati kutoa usaidizi wa kibinadamu wa kuokoa maisha na kusaidia watu wa Sudan katika matarajio yao ya mustakabali wenye amani na usalama. 

Sauti
1'57"