Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashambulizi na umwagaji damu vinaendelea Gaza licha ya kuanza kwa Ramadhan mauaji - Guterres

Mashambulizi na umwagaji damu vinaendelea Gaza licha ya kuanza kwa Ramadhan mauaji - Guterres

Pakua

Leo ni mwanzo wa mwezi mktukufu wa Ramadhan ambapo Waislamu kote duniani husherehekea na kuchagiza tunu za amani, maridhiano na mshikamano lakini uhasama unaendelea hususani sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Gaza ambako mauaji , na mashambulizi hayajakoma amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani hii leo. 

Hivyo ndivyo alivyoanza Katibu Mkuu katika tarifa yake fupi kwa waandishi wa habari akikumbusha kuwa ni hivi majuzi tuliingia mwezi wa sita tangu shambulio la kigaidi la Hamas nchini Israel na mashambulizi mabaya ya Israel huko Gaza. 

Ameo leo ana ombi kubwa ambalo ni “kuheshimu dhamira ya Ramadhani kwa kunyamazisha mtutu wa bunduki na kuondoa vikwazo vyote ili kuhakikisha utoaji wa misaada ya kuokoa maisha kwa kasi na kiwango kikubwa kinachohitajika.”

Pia ametaka wakati huohuo kwa kuzingatia dhamira ya Ramadhani kuwaachilia mateka wote wanaoshikiliwa mara moja. 

Katibu Mkuu ameonya kwamba “Macho yadunia yanatazama. Macho ya historia yanatazama. Hatuwezi kuyapa kisogo yanayoendelea ni lazima tuchukue hatua kuepusha vifo vinavyoweza kuzuilika.” 

Amesema Dunia imeshuhudia mwezi baada ya mwezi mauaji ya raia na uharibifu wa miundombinu ya raia kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea katika miaka yangu yote akiwa Katibu Mkuu. 

Na kwamba msaada wa kuokoa Maisha kwa raia Gaza unaingia kwa vikwazo vikbwa na wakati mwingine hauingii kabisa.

Amesema hivi sasa Sheria ya kimataifa za kibinadamu ziko katika hali mbaya.Na tishio la Israel kushambulia Rafah zinaweza kuwatumbukiza kuzimu zaidi watu wa Gaza.

Amesema pamoja na kwamba viongozi wa Dunia na wahudumu wa kibinadamu wamekuwa wakitoa wito wa kusitishwa mapigano wito mahsusi umetoka kwa familia za waathirika wa vita hivi. 

Sitasahau mikutano yangu pamoja nao na wamesimama kwenye jukwaa hili na kukuhutubia wameungana kwa ujasiri mkubwa na maumivu yasiyopimika. 

Familia za mateka wa Israeli ambao wameeleza mateso na uchungu wao na wameomba kuachiliwa mara moja kwa wapendwa wao. 

Pia alikutana na familia za waathirika wa Gaza ambazi zimeomba uhasama kutishishwa mara moja “Kama mmoja wa wanafamilia hao alisema, Hatuko hapa kwa ajili ya rambirambi. Hatupo hapa kwa ajili ya kuomba msamaha. Tuko hapa kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za haraka. Je, hili ni kubwa sana kuliomba? Ni lazima tusikilize na kutii sauti hizo.” Amesesisitiza Guterres. 

Pia amesema leo anatoa ombi la usitishaji uhasama Sudan kwa ajili ya Ramadhani na kukumbusha kwamba hivi karibuni mwezi Aprili kutakuwa na Sikukuu za Pasaka na sikukuu ya Wayahudi ya Passover hivyo huu ni wakati wa kuonyesha huruma, kuchukua hatua na kurejesha Amani.

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
2'53"
Photo Credit
UNTV