Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IFAD: Mradi wa ukulima nchini Malawi waboresha maisha ya na usawa kijinsia katika jamii

IFAD: Mradi wa ukulima nchini Malawi waboresha maisha ya na usawa kijinsia katika jamii

Pakua

Nchini Malawi Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya Kilimo IFAD unatekeleza mradi wa kuwasaidia wanawake wa vijijini kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia na sasa wananachi wanafaidi matunda yake. 

Mradi huo uitwao TRADE ulioanzishwa mwaka 2022 na serikali ya Malawi kwa kushirikiana na IFAD inalenga kubadilisha kilimo kupitia mpango wake wa Mseto na Ujasiriamali. 

Amos Mailosi ni Afisa Mazingira wa kanda Mabadiliko ya Tabianchi wa mradi huo wa TRADE na anasema jambo muhimu katika mradi wao ni kuhakikisha familia zinafanya kazi na kufikia maamuzi pamoja. 

“Moja ya eneo muhimu katika programu yetu ya TRADE ni kuhamasisha suala la ushirikishwaji wa kijinsia ndani ya jamii. Kwa hivyo, tunajaribu kuwawezesha wanawake na wanaume, na wavulana na wasichana, kushiriki kwa usawa katika afua. Ili kwa pamoja waweze kutambua umuhimu wa kufanya maamuzi ya pamoja katika ngazi ya kaya.”

Kwa miaka mwili sasa mafanikio yameanza kuoneskana, na mmoja wa wanufaika hao ni Alefu Ofesa na mume wake Lloyd ambao wamekuwa wakulima kwa miaka 20 lakini kwa takriban miaka miwili wamebadili kilimo kuwa biashara. Mabadiliko haya yamefuatitia Alefa na wanawake wenzake kijijini kupatiwa Msaada na mafunzo ya mbinu mpya za kilimo ambazo zimewasaidia kukabiliana na mvua zisizokuwa na uhakika katika ukanda huo. 

“Mradi huu umekuwa ukihimiza wanawake kushiriki katika kilimo. Kwa ujuzi na maarifa tuliyopatiwa tuna uhakika kuhusu kile kinachohitajika kufanywa ili kuboresha uzalishaji, kwa mfano upandaji kwa kutumia mistari miwili. Wanawake wengi hapa sasa ni wataalam wa shughuli za kilimo na kwa sababu ya faida wanazopata, wengi wametambua umuhimu wa kujiunga pamoja.”

Alefa amepanga kutumia mapato ya ziada wanayopata kwa ajili ya kuwapatia elimu watoto wao na kununua kigari cha ng'ombe kwa ajili ya usafiri. 

Sio tu kwamba familia yake sasa ina chakula cha kutosha kwa mwaka mzima, lakini sasa anaweza pia kuuza sehemu ya kile anachovuna, na anapanga kupanua biashara yake ili kuuza kwenye masoko katika vijiji vya jirani.

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
2'18"
Photo Credit
© CIAT/Neil Palmer