Takriban wakimbizi 100,000 wanaowasili Uganda wanakabiliwa na mahitaji makubwa
Huku kukiwa na ongezeko la mahitaji ya kibinadamu kwa wakimbizi 96,000 ambao wamekimbilia Uganda hadi sasa mwaka huu, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR na wadau wanahitaji haraka dola za Marekani milioni 68 kwa ajili ya usaidizi na huduma za kuokoa maisha.