Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Sudan Kusini

Wakimbizi wa ndani katika jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini.
UNMISS

Makabidhiano ya mamlaka kwa njia ya amani, kidemokrasia na kwa wakati, bado ni muhimu Sudan Kusini - Haysom

Huku Sudan Kusini ikikabiliana na changamoto nyingi za wakati mmoja, Nicholas Haysom, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na ambaye pia ni Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS amewataka viongozi wa kisiasa kuongeza kasi katika mchakato wa amani unaoendelea ili uchaguzi huru, haki na wa kuaminika uwezekufanyika kwa wakati. 

Wananchi wa Sudan Kusini washerehekea tamasha la utamaduni la amani katika mji wa Aweil.
UNMISS

Tamasha la utamaduni wa amani layaleta pamoja makabila ya Sudan Kusini

Mwanzoni mwa mwezi huu wa April dunia iliadhimisha Siku ya Kimataifa ya michezo kwa maendeo na amani, nchini Sudan Kusini kwa siku mbili mfululizo maelfu ya wananchi wa walikusanyika kusherehekea tamasha la utamaduni la amani lililoandaliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni ya jimbo la Kaskazini la Bahr El Ghazal.

Sauti
4'27"
Mlinzi wa amani wa UNMISS nchini Sudan Kusini akishika doroa kwenye jimbo la Equatorial
UN Photo/Isaac Billy

Raia wa Sudan Kusini walikatiliwa na kuuawa Zaidi mwaka 2022 ikilinganishwa na 2021: UNMISS

Mpango wa umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini UNMISS leo umetoa taarifa ya kila mwaka ya haki za binadamu na ukatili unaoatjiri raia ambayo inaonyesha kuna ongezeko la asilimia 2 la idadi ya raia waliokatiliwa nchini humo mwaka 2022, licha ya kupungua kwa vitendo vya ukatili kwa ujumla kwa asilimia 27 mwaka 2022 ikilinganisha na mwaka 2021.

Watu walioyakimbia makazi yao katika eneo la Equatoria Magharibi Sudan Kusini wakikutana na viongozi wa vijiji.
UNMISS

Maelfu ya wakimbizi wa ndani wa Tambura warejea makwao

Sudan Kusini ni moja ya nchi iliyoathirika kwa muda mrefu na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo mara kwa mara makundi ya wapiganaji wenye silaha yalikuwa yakivamia katika vijiji na kuwaua raia na kupora mali zao. Kutokana na sababu hiyo wananchi wengi wamekuwa wakikimbilia katika kambi za kijeshi zilizoko karibu na maeneo yao ili kusaka hifadhi.

Sauti
4'9"
Mapigano ya kikabila katika eneo la Jonglei nchini Sudan Kusini yamesababisha utekaji nyara na mauaji. (Maktaba))
UNMISS

UNMISS na wadau wa kimataifa wahofia kuendelea kwa vurugu Greater Pibor na Jonglei

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS, mpango wa Muungano wa Afrika Sudan Kusini AUMISS, IGAD, Troika, Muungano wa Ulaya EU na R-JMEC wamesema wana wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa ghasia, kupoteza maisha na ripoti za madai ya matumizi ya silaha nzito katika Eneo la Utawala la Greater Pibor na vijana wenye silaha kutoka jimbo la Jonglei.