Siku ya nishati COP26 yasikia vilio vya kutaka makaa ya mawe yasalie historia

Mwanaharakati akiwa amevalia kama kikaragosi Pikachu wakiandamana nje ya ukumbi wa mikutano COP26
UN News/Laura Quinones
Mwanaharakati akiwa amevalia kama kikaragosi Pikachu wakiandamana nje ya ukumbi wa mikutano COP26

Siku ya nishati COP26 yasikia vilio vya kutaka makaa ya mawe yasalie historia

Tabianchi na mazingira

Katika siku ya nne ya mkutano wa 26 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP26 huko Glasgow, Scotland, sauti zimepazwa na wanaharakati wakitaka kukomeshwa kwa matumizi ya makaa ya mawe nishati ya gesi na mafuta, sauti ambazo zimepaswa siku ambayo mkutano huo ulikuwa unamulika nishati.

Wajumbe kwenye mkutano huo leo wamekariri maneno ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, “makaa ya mawe yasalie historia.”

Rais wa mkutano huo wa COP26 Alok Sharma ametangaza taarifa ya kipindi kipya duniani cha mpito wa kuelekea nishati safi na salama, ahadi ambayo ni ya kumaliza matumizi ya makaa ya mawe na kuimarisha matumizi ya nishati salama wakati wa kipindi cha mpito huku nishati haribifu kwa mazingira yakiwemo makaa yam awe yakikoma katika nchi tajiri mwaka 2030 na kwingineko mwaka 2040.

Tamko hilo la ahadi limetiwa saini nan chi 77, zikiwemo 46 kama vile Poland, Vietnam na Chile, 23 kati yao zikiahidi kwa mara kwanza kuacha matumizi ya makaa ya mawe.

“Yote haya yanasaidia dunia kuondokana kabisa na uzalishaji wa hewa chafuzi. Tunafahamu hatua zaidi zinapaswa kuchukuliw na ni juu ya serikali, sekta ya biashara, taasisi za fedha na mashirika ya kijamii  na tunapaswa kuendelea kusongesha kasi hii ya ushirikiano. Ninaamini kuna matumaini ya kuondokana na makaa ya mawe na ninaamini tutafikia hatua ambapo nishati ya makaa yam awe itakuwa historia,” amesema Bwana Sharma akihutubia mjadala kuhusu nishati.

Kwa bahati mbaya, tamko hilo la ahadi halijumuishi wafadhili wakubwa wa makaa ya mawe duniani ambao ni China, Japan, Korea Kusini ambazo hata hivyo mwaka jana ziliahidi kuwa zitaacha ufadhili wa uzalishaji wa makaa ya mawe ugenini ifikapo mwishoni mwa mwaka huu wa 2021.

Hewa mbadala kama hii inayotokana na upepo ni muhimu katika kutokomeza uchafuzi wa hewa kwenye shamba Montenegro.
Unsplash/Appolinary Kalashnikova
Hewa mbadala kama hii inayotokana na upepo ni muhimu katika kutokomeza uchafuzi wa hewa kwenye shamba Montenegro.

Wakati huo huo, ushirika unaolenga kuondokana na matumizi ya nishati ya makaa ya mawe kiendelevu, kiuchumi na kijumuishi au Powering Past Coal Alliance, umekaribisha wanachama wapya hii leo wakijumuisha nchi 7 na taasisi 14 za kifedha.

Hapo jana serikali za Afrika Kusini, Ufaransa, Ujerumani na Uingereza pamoja na Muungano wa Ulaya walitangaza mipango mipya mikubwa na ya muda mrefu ya ubi awa mpito wa kuondokana na hewa ya ukaa kuunga mkono hatua za Afrika Kusini. Rais wa Marekani Joe Biden na Kamishna wa Muungano wa Ulaya Ursula Von de-Leyen walizungumza kwa njia ya mtandao kutoa tangazo hilo wakati hii leo wakati wa tukio la nishati.

Haitoshi

Wakati ikielezwa kuwa ahadi zinatia moyo, wawakilishi wa mashirika ya kiraia wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano wanasema hawaelewi na haitoshi.

Katika mitakuno tofauti na wanahabari, shirika la kiraia la Ujerumani Urgewald na mtandao wa hatua kwa tabianchi wameelezwa kukata tamaa kutokana na janga la sasa la nishati.

“Katika miaka miwili iliyopita, tumeshuhudia kuongezeka kwa sera za makaa ya mawe lakini hakuna chochote kuhusu gesi na mafuta. Sababu ya hilo ni kwamba taasisi za fedha ambazo zinataka kuondokana na nishatiya mafuta kisukuku zinakumbwa na tatizo kubwa ambalo ni ukosefu wa taarifa,” amesema mwendesha kampeni wa masuala ya fedha kutoka shirika la kiraia la Urgewald.

Shirika la haki za binadamu na mazingira limechapisha takwimu zao mpya zinazoonesha kuwa wazalishaji 506 wa mafuta na gesi wamepanga kuongeza mapipa bilioni 190 ya mafuta na gesi sawa na kiwango chao za uzalishaji kwa sasa katika kipindi cha mwaka 1 hadi 7 ijayo.

“Angalau asilimia 96 ya wazalishaji wa gesi na mafuta wanapanga kuongeza mali zao,” ameongeza mwakilish iwa Urgewald, akisema sekta hiyo iko katika mipango ya kupanua uzalishaji wao na kuweka miradi imipya.

Wakati huo huo, Jing Zhu, Mkurugenzi wa programu ya miradi ya nishati safi kwa mazingira amesisitiza kuwa hatuna tena muda wa nishati ya mafuta kisukuku.

“Tumeshuhudia nchi za kundi 20 au G20 zikienda upande tofauti. Kuanzia mwaka 2018-2020 nchi za G20 ziliahidi dola bilioni 188 kwa mafuta ya kisukuku. Hii ni mara 2.5 zaidi ya kiwango wanachoweka katika nishati rejelevu na hii ni hatari sana,”  Amesema Bi. Zhu.

Ahadi mpya

Bi. Ms. Zhu, hata hivyo ametangaza kwa tahadhari taarifa mpya wakati akizungumza waandishi wa habari.
Kundi la serikali na taasisi za umma za fedha duniani kote ukiwemo Muungano wa Ulaya, Canada na Uingereza zimeahidi kuachana na uungaji mkono harakati za uzalishaji wa nishati ya mafuta kisukuku ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao wa 2022.