Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

DR Congo

Askari wa kikosi cha FIB akishika doaria  Beni Mashariki mwa DRC ambapo UN ilikuwa inasaidia jeshi la serikali katika operesheni zake.
Photo: MONUSCO/Sylvain Liechti

Mashambulizi dhidi ya raia yaongezeka Beni: UNHCR

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR limesema lina wasiwasi kuhusu usalama wa maelfu ya raia katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, DRC ambako ghasia za makundi yenye silaha zimeongezeka na za hivi karibuni zimesababisha vifo vya watu zaidi ya 20. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

Maafisa wa afya wakisafishwa dhidi ya virusi vya Ebola baada ya kuwatembelea wagonjwa katika vituo vya matibabu mjini Butembo DRC.
© UNICEF/UN0235950/Nybo

Tuna wasiwasi na mayatima wa Ebola DRC:UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia watoto, UNICEF likishirikiana   na washirika wao linasema limeorodhesha  watoto 155 ambao wamepoteza wazazi wao au waliachwabila mlezi kutokana na  mlipuko ugonjwa wa Ebola  uliotokea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.