Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UDHR70

UDHR70
Tamko la Haki za Binadamu la UN-Uchambuzi wa Ibara

Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, UDHR, ni nyaraka ya kihistoria iliyopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 1948 kwa lengo la kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa. Rasimu ya nyaraka hii iliandaliwa na wawakilishi wenye usuli tofauti kuanzia sheria hadi utamaduni na walitoka maeneo yote ya dunia. Baada ya kuiandaa na kuijadili rasimu hiyo ilipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 10 Disemba mwaka 1948 mjini Paris, Ufaransa kwa azimio namba 217 A la baraza hilo. Likipatiwa jina la tamko la haki za binadmu, nyaraka hiyo inaweka viwango vya pamoja vya haki za binadamu kwa wote na mataifa yote. Azimio hilo, kwa mara ya kwanza liliweka misingi ya haki za binadamu inayokubalika kimataifa na inayopaswa kulindwa popote pale duniani. Hadi sasa nyaraka hiyo imetafsiriwa kwa zaidi ya lugha 500 ikiwemo Kiswahili.

Pata taarifa kila wakati pindi tunapochapisha taarifa mpya kwa kujisajili

Photo UNAMA / Abbas Naderi

Kubadili mifumo ndio muarobaini wa haki za huduma za jamii Tanzania: Dkt.Bisimba

Nchini Tanzania ingawa katika katiba  imeaainishwa haki za huduma za jamii kwa wote, mifumo iliyopo inafanya kuwa changamoto kubwa ya utekelezaji wa haki hizo. Hayo yamesemwa na Dkt.Helen Kijo Bisimba mwanaharakati wa muda mrefu wa haki za binadamu nchini humo. Akijadili ibara ya 21 ya tamko la haki za binadamu  isemayo “kila mtu ana haki ya kushiriki katika serikali yake, haki sawa za huduma za jamii ikiwa ni pamoja na serikali kuongoza kwa matakwa ya wananchi”, Dkt.

Sauti
5'29"

29 Novemba 2018

Leo katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa Arnold Kayanda anakuletea

-Hatari ya VVU kwa vijana barubaru ifikapo 2030, barubaru 80 watapoteza maisha kila siku kama mwenendo hautobadilika limeonya shirika la UNICEF

-Umuhimu wa ushirika wa Kusini-Kusini kwa bara la Afrika ni mkubwa

-UNMISS kuongeza vikosi jimbo la Nile Sudan Kusini kwa ajili ya ulinzi wa raia

-Makala inamulika Ibara ya 21 ya tamko la haki za binadamu kuhusu "haki ya wananchi kushiriki katika serikali , huduma za jamii na uongozi kuzingatia matakwa ya wananchi".

Sauti
14'4"

Katu mtu asilazimishwe kujiunga na chama hata ndani ya familia- Wakili Komba

Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambalo mwaka  huu linatimiza miaka 70 tangu kuasisiwa lina ibara 30 ambazo ni msingi wa haki za binadamu kote duniani. Licha ya kuwepo kwa muda mrefu baadhi ya haki zinasiginwa katika baadhi ya maeneo na sababu kuu ni kwa wanachi kutofahamu vyema haki zao. Ni kwa msingi tumekuwa tunakuletea uchambuzi wa Ibara kwa Ibara ambapo leo Wakili Aloyce Komba kutoka Tanzania amezungumza na Arnold Kayanda wa Idhaa hii akifafanua ibara ya 20.

Audio Duration
4'18"
Pakaza rangi ya chungwa! Angazia haki za wanawake na wasichana na kataa ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.
UN Women

Ukatili dhidi ya wanawake ni fedheha kwa jamii zote:Guterres

Ukatili dhidi ya wanawake na wasichana ni ugonjwa wa kimataifa unaoleta fedheha kubwa katika jamii zote duniani . Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake maalumu kuhusu siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake ambayo huadhimishwa kila mwaka Novemba 25.

©UNHCR/O. Akindipe

Baadhi ya watu hunyimwa haki yao ya kumiliki mali

Katika mwendelezo wa kupitia ibara za tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambalo mwaka huu wa 2018 linatimiza miaka 70, leo inamulikwa ibara ya 17 inayozungumzia haki ya mtu kumiliki mali yeye mwenyewe au kwa ushirika na mtu mwingine au wengine. Ibara hii inazingatia ukweli kwamba baadhi ya watu wananyimwa haki hiyo kwa misingi mbalimbali ikiwemo rangi, jinsia, kabila, dini au umri. Katika basi kuangazia utekelezaji wa ibara hiyo tunajikita katika mtu kunyimwa haki hiyo kwa misingi ya kijinsia na kutufafanulia hayo ungana na Siraj Kalyango katika makala hii.

Sauti
3'17"

Jinamizi la kutosajiliwa utotoni, laandama maelfu ya watu wasio na utaifa

Ibara ya 15 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linasisitiza haki ya mtu kuwa na utaifa. Iwe ni utaifa kwa kuzaliwa au kwa kusajiliwa katika nchi nyingine. Hata hivyo kutokana na sababu mbalimbali zaidi ya watu milioni 12 hivi sasa duniani  hawana utaifa. Ukosefu wa utaifa  unapoka watoto na watu wazima haki zao za msingi. Je ni sababu gani basi zinafanya watu wakose utaifa, na ni madhila yapi basi wanapitia? Ungana basi na Grace Kaneiya katika makala hii.

Sauti
3'11"