Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kubadili mifumo ndio muarobaini wa haki za huduma za jamii Tanzania: Dkt.Bisimba

Kubadili mifumo ndio muarobaini wa haki za huduma za jamii Tanzania: Dkt.Bisimba

Pakua

Nchini Tanzania ingawa katika katiba  imeaainishwa haki za huduma za jamii kwa wote, mifumo iliyopo inafanya kuwa changamoto kubwa ya utekelezaji wa haki hizo. Hayo yamesemwa na Dkt.Helen Kijo Bisimba mwanaharakati wa muda mrefu wa haki za binadamu nchini humo. Akijadili ibara ya 21 ya tamko la haki za binadamu  isemayo “kila mtu ana haki ya kushiriki katika serikali yake, haki sawa za huduma za jamii ikiwa ni pamoja na serikali kuongoza kwa matakwa ya wananchi”, Dkt. Bisimba amesema , kuzungumzia  na kuorodhesha haki kwenye kataratasi ni suala moja , lakini kuzitekeleza ipasavyo ni suala lingine. Hata hivyo akianza kwa kufafanua utekelezaji wa haki za ushiriki wa wannachi katika serikali amesema suala hilo lina pande mbili

Audio Credit
Anold Kayanda/Flora Nducha
Audio Duration
5'29"
Photo Credit
Photo UNAMA / Abbas Naderi