Jinamizi la kutosajiliwa utotoni, laandama maelfu ya watu wasio na utaifa
Pakua
Ibara ya 15 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linasisitiza haki ya mtu kuwa na utaifa. Iwe ni utaifa kwa kuzaliwa au kwa kusajiliwa katika nchi nyingine. Hata hivyo kutokana na sababu mbalimbali zaidi ya watu milioni 12 hivi sasa duniani hawana utaifa. Ukosefu wa utaifa unapoka watoto na watu wazima haki zao za msingi. Je ni sababu gani basi zinafanya watu wakose utaifa, na ni madhila yapi basi wanapitia? Ungana basi na Grace Kaneiya katika makala hii.
Audio Credit
Anold Kayanda/Grace Kaneiya
Audio Duration
3'11"