Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN Women /Aidah Nanyonjo

Wanawake waimarisha ushiriki kwenye siasa za Uganda

Kufuatia juhudi za shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women za kuwezesha wanawake, kupitia wadau mbalimbali duniani kote, kumekuwa na hatua chanya katika nchi kadhaa zikiwemo zile za Afrika Mashariki.

Kwa sasa ni bayana kwamba wanawake wanajitokeza kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa na mara nyingine kuwashinda wanaume hali hiyo ikiwa ni tofauti na zamani ambapo ulikuwa ni mwiko kwa mwanamke kusimama mbele hadharani na kuongea.

Sauti
3'47"
World Bank/Maria Fleischmann

Tumenufaika sana na mafunzo ya lishe endelevu-Morogoro

Wanawake 40 na wanaume 21 wamenufaika na mafunzo kuhusu lishe endelevu, mafunzo ambayo yamefanyika katika eneo la Mvomero, Turiani Morogoro Tanzania kwa usimamizi wa shirika la Save the Children. John Kabambala wa redio washirika Kids Time FM amewahoji baadhi yao wakieleza mafunzo yalivyowasaidia na kuwa watayatumia kwenda kuelimisha wengine katika maeneo yao. 

Audio Duration
3'43"
UN/Imani Nsamila

Kuna pengo kubwa kati ya wanaume na wanawake kwenye tasnia ya upigaji picha Tanzania -Nsamila

Nchini Tanzania, mpiga picha maarufu, Imani Nsamila kwa kushirikiana na shirika la Ladies Joint Forum na Kikoi innovative media, kwa siku tano wamewapa mafunzo ya upigaji picha wasichana 28 ikiwa ni moja ya harakati za kuyafikia malengo Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu, SDGs, kama vile lengo namba 5 linalolenga ulimwengu kuwa na usawa wa kijinsia kufikia mwaka 2030. Ahimidiwe Olotu wa Kituo cha habari cha  Umoja wa Mataifa UNIC Dar es Salaam amemhoji Imani Nsamila ambaye anaanza kwa kueleza alisukumwa na nini kuanza na kundi hili? 

 

Sauti
3'24"
UN/ John Kibego

COVID-19 yamuondoa mwimbaji jukwaani na kumrejesha kwenye useremala

COVID-19 imekuwa na madhara makubwa kwa vijana kote duniani kuanzia kipato hadi ustawi wa kijamii kutokana na wengi wao kupoteza ajira.

Hali hii ambayo imedumu kwa miezi nane sasa katika baadhi ya nchi imewalazimu vijana kuwa wabunifu zaidi na kutafuta njia mbadala za kipato ili kuepuka kuepuka maisha magumu.

Nchini Uganda, kijana mwimbaji Gerald Mutabaazi  aliamua kukimbilia msituni na kuanza sanaa ya kutengeneza vifaa vya upishi ili mikono ya wanafamilia yake iende kinywani.

Sauti
3'44"
UN/Rose Nyabhate

Safari ya wasichana na wanawake kuingia kwenye kiwanda cha uchekeshaji Kenya, haikuwa rahisi-Nyabheta 

Taaluma ya ugizaji inaendelea kubadilika kila uchao katika nyakati ambazo teknolojia ya mawasiliano inazidi kukua.  Nchini Kenya kwa sasa, tasnia ya uigizaji na uchekeshaji imeajiri vijana wengi wa kiume na wa kike ingawa safari ya kundi moja kati ya hayo mawili haikuwa rahisi. Je wanawake wamechukua nafasi gani katika taaluma ya uigizaji na uchekeshaji kwa sasa? Jason Nyakundi amezungumza na mchekeshaji wa miaka mingi wa vipindi vya televisheni nchini Kenya Rose Nyabhate  kutaka kujua safari yake imekuwa ya aina gani katika tasnia hii. 

Sauti
3'36"
UN News/ John Kibego

Kwa sasa nimewaambia wakimbizi wenzangu tusishikane mikono, tusitembeleane- Acces Bazibuha  

Sasa ni makala ambapo tunafuatilia hali ilivyo na mikakati inayowekwa na wadau mbalimbali yakiwemo mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR, la afya WHO na wizara ya afya ya nchini hiyo kuzuia kuenea kwa COVID-19 kufuatia mlipuko wake katika makazi ya wakimbizi ya Kyangwali na kusababisha kifo cha mkimbizi mmoja hapo tarehe nane Agosti mwaka huu. Moja ya hatua ilikuwa ni kuzuia watu kutembea huku na kule, na pia kufuatilia watu waliokutana na mkimbizi aliyeambukizwa. 

Sauti
54"
© UNICEF/Zahara Abdul

Maziwa ya ng'ombe yana protini isiyoweza kumeng'enywa kwenye tumbo la mtoto mwenye umri wa chini ya miezi 6 - Mtaalamu

Ni mwaka mmoja tangu mradi wa mafunzo kuhusu lishe endelevu ulipoanzishwa mkoani Morogoro kwa ufadhili wa shirika la Save the Children na shirika la Marekani la msaada wa kimataifa USAID. Sehemu ya mradi huo ni kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa mtoto kunyonya maziwa halisi ya mama angalau kwa miezi sita ya kwanza. Je, wanuafaika wa mradi huo wanasemaje? Wameelimika kwa kiasi gani tangu mradi huo kuanzishwa mwezi Agosti mwaka jana 2019? John Kabambala wa redio washirika Kids Time FM amezungumza nao na kuandaa makala hii. 

Sauti
3'25"
UN/ Jason Nyakundi

Nchini Kenya vijana wabuni kifaa cha kunawa mikono kwa urahisi kujikinga na virusi vya Corona

Leo ni siku ya kimataifa ya vijana kaulimbiu mwaka huu ikiwa "ujumuishwaji wa vijana kwa ajili ya hatua za kimataifa" Umoja wa Mataifa ukisisitiza kuwa kundi hilo la watu katika jamii linaweza kuwa na mchango mkubwa katika kutatua changamoto zinazoikabili duniani hivi sasa. Nchini Kenya vijana wengi wameitikia wito wa kujumuishwa katika hatua za masuala ya kimataifa ikiwemo vita dhidi ya janga la corona au COVID-19 ambalo linaendelea kuitikisa dunia kwa sasa.

Sauti
5'27"
UN Tanzania/Ahimidiwe Olotu

Asante UNIC Dar es Salaam kunipa fursa ya kukuza maarifa yangu-Hilda Amedhastone Phoya

Je una ndoto za siku moja kufanya kazi na Umoja wa Mataifa? Makala ifuatayo ni mahojiano kati ya Ahimidiwe Olotu wa UNIC Dar es Salaam na Hilda Amedhastone Phoya, mwanafunzi ambaye amehitimisha mafunzo kwa vitendo katika Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC Dar es Salaam, akieleza kuhusu alivyonufaika na fursa ya kujifunza kwa vitendo katika kituo hicho kinachohusika na habari za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na jinsi kituo hicho kilivyonoa uelewa wake kuhusu masuala mbalimbali ya kimataifa. 

Sauti
3'39"
UNEP/Natalia Mroz

Wanyama wahatarisha usalama wa chakula kati nya COVID-19, Uganda

Wanyama ni sehemu muhimu ya mazingira na pia uwepo wao hutegemea mazingira sawa na binadamu. Lakini uchafuzi wa mazingira kutokana na ongezeko la idadi ya watu na baadhi ya watu kutojali maana ya misitu na maeneo mengine, makaazi ya wanyama yamechafuliwa na kuchochea mzozo kati ya binadamu na wanyama ambapo uhakika w achakula umeigia hatarini zaidi hasa kwa jamii jirani za mbuga za wanyamapori nchini Uganda.

Sauti
3'50"