Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanyama wahatarisha usalama wa chakula kati nya COVID-19, Uganda

Wanyama wahatarisha usalama wa chakula kati nya COVID-19, Uganda

Pakua

Wanyama ni sehemu muhimu ya mazingira na pia uwepo wao hutegemea mazingira sawa na binadamu. Lakini uchafuzi wa mazingira kutokana na ongezeko la idadi ya watu na baadhi ya watu kutojali maana ya misitu na maeneo mengine, makaazi ya wanyama yamechafuliwa na kuchochea mzozo kati ya binadamu na wanyama ambapo uhakika w achakula umeigia hatarini zaidi hasa kwa jamii jirani za mbuga za wanyamapori nchini Uganda.

Kuna hofu kuwa wakati uchumi umedorora juu ya COVID-19, mzozo utaongezeka na kuathiri binadamu na wanyama ikiwa juhudi zaidi hazitafanywa kurejesha uwiano.

Je, kulikoni?Basi ungana na John Kibego aliyezungumza na William Bamuturaki mwanajamii za mbuga ya wanyamapori ya Murchson Falls.

Audio Credit
Loise Wairimu\John Kibego
Audio Duration
3'50"
Photo Credit
UNEP/Natalia Mroz