COVID-19 imenirudisha nyumbani kijijini-Waweru
Tangu lizuke janga la corona duniani athari nyingi za karibu kila sekta zimeshuhudiwa. Vijana ambao idadi yao ndiyo kubwa kwa karibu kila nchini duniani nao wameathirika pakubwa. Wengi walilazimika kusitisha masomo kufuatia kufungwa shule na taasisi za elimu, wengine wakapoteza ajira na kubaki katika hali ya sintofahamu kuhusu hatma ya maisha yao. Kijana Joseph Waweru alipoteza kibarua chake mjini Nairobi na pia mipango yake ya masomo katika chuo kikuu ikakwama ndipo akaamua kuhamia kwao alikozaliwa huko Kitale, magharibi mwa Kenya.