Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchini Kenya vijana wabuni kifaa cha kunawa mikono kwa urahisi kujikinga na virusi vya Corona

Nchini Kenya vijana wabuni kifaa cha kunawa mikono kwa urahisi kujikinga na virusi vya Corona

Pakua

Leo ni siku ya kimataifa ya vijana kaulimbiu mwaka huu ikiwa "ujumuishwaji wa vijana kwa ajili ya hatua za kimataifa" Umoja wa Mataifa ukisisitiza kuwa kundi hilo la watu katika jamii linaweza kuwa na mchango mkubwa katika kutatua changamoto zinazoikabili duniani hivi sasa. Nchini Kenya vijana wengi wameitikia wito wa kujumuishwa katika hatua za masuala ya kimataifa ikiwemo vita dhidi ya janga la corona au COVID-19 ambalo linaendelea kuitikisa dunia kwa sasa. Na miongoni mwa mchango wa vijana hao ni kuvumbua vifaa mbalimbali vya kusaidia vita dhidi ya gonjwa hilo katika jamii zao. Leo mwandishi wetu wa Kenya Jason Nyakundi  ameangazia eneo la Thika nchini humo ambako vijana watatu wamevumbua kifaa kinachowasaidia watu kutakasa mikono bila ya kuguswa au (Automatic hand sanitizer dispenser) ambacho kimeanza kupata umaarufu kwa kasi na kuzungumza na mmoja wa wavumbuzi hao Bernad Kagwe ambaye anaeleza nini kiliwasukuma kuvumbua kifaa hicho

Audio Credit
Loise Wairimu\Jason Nyakundi
Audio Duration
5'27"
Photo Credit
UN/ Jason Nyakundi