Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COVID-19 yamuondoa mwimbaji jukwaani na kumrejesha kwenye useremala

COVID-19 yamuondoa mwimbaji jukwaani na kumrejesha kwenye useremala

Pakua

COVID-19 imekuwa na madhara makubwa kwa vijana kote duniani kuanzia kipato hadi ustawi wa kijamii kutokana na wengi wao kupoteza ajira.

Hali hii ambayo imedumu kwa miezi nane sasa katika baadhi ya nchi imewalazimu vijana kuwa wabunifu zaidi na kutafuta njia mbadala za kipato ili kuepuka kuepuka maisha magumu.

Nchini Uganda, kijana mwimbaji Gerald Mutabaazi  aliamua kukimbilia msituni na kuanza sanaa ya kutengeneza vifaa vya upishi ili mikono ya wanafamilia yake iende kinywani.

Hii ilikuwa baada ya pato kutoka uimbaji kufifizwa na vikwazo vya kudhibiti COVID-19. Je, anafanyaje? Uungana na Joh Kibego katika makala ifuatayo.

Audio Credit
Loise Wairimu/ John Kibego
Audio Duration
3'44"
Photo Credit
UN/ John Kibego