Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kwa sasa nimewaambia wakimbizi wenzangu tusishikane mikono, tusitembeleane- Acces Bazibuha  

Kwa sasa nimewaambia wakimbizi wenzangu tusishikane mikono, tusitembeleane- Acces Bazibuha  

Pakua

Sasa ni makala ambapo tunafuatilia hali ilivyo na mikakati inayowekwa na wadau mbalimbali yakiwemo mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR, la afya WHO na wizara ya afya ya nchini hiyo kuzuia kuenea kwa COVID-19 kufuatia mlipuko wake katika makazi ya wakimbizi ya Kyangwali na kusababisha kifo cha mkimbizi mmoja hapo tarehe nane Agosti mwaka huu. Moja ya hatua ilikuwa ni kuzuia watu kutembea huku na kule, na pia kufuatilia watu waliokutana na mkimbizi aliyeambukizwa. 

Mwandishi wetu John Kibego amezungumza na Access Bazibuha Mudosia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambaye anajitahidi kuzingatia maagizo mapya yanayotolewa kukabiliana na janga hilo na hatua anazozichukua mwenyewe. 

Audio Credit
Loise Wairimu/John Kibego
Audio Duration
54"
Photo Credit
UN News/ John Kibego