Janga la COVID-19 halikumzuia mzazi Ghana kuhakikisha watoto wanaendelea kujifunza
Nchini Ghana, janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 lililoibuka mwezi Machi mwaka jana wa 2020 lilitikisa shughuli za kisiasa, kiuchumi na kijamii. Mathalani shule zilifungwa na hivyo kutikisa pia ari ya wazazi waliokuwa wakijitolea kufundisha hasa katika shule zilizoko vijijini. Mwelekeo wa kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hususan namba 4 kuhusu elimu bora ulikuwa mashakani. Wazazi walishajitolea kusaidia maeneo ya vijijini lakini kufungwa kwa shule kukaleta hofu.