Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Janga la COVID-19 halikumzuia mzazi Ghana kuhakikisha watoto wanaendelea kujifunza

Janga la COVID-19 halikumzuia mzazi Ghana kuhakikisha watoto wanaendelea kujifunza

Pakua

Nchini Ghana, janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 lililoibuka mwezi Machi mwaka jana wa 2020 lilitikisa shughuli za kisiasa, kiuchumi na kijamii. Mathalani shule zilifungwa na hivyo kutikisa pia ari ya wazazi waliokuwa wakijitolea kufundisha hasa katika shule zilizoko vijijini. Mwelekeo wa kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hususan namba 4 kuhusu elimu bora ulikuwa mashakani. Wazazi walishajitolea kusaidia maeneo ya vijijini lakini kufungwa kwa shule kukaleta hofu. Ingawa hivyo wazazi hao walitumia mbinu nyingine ya kutembea nyumba hadi nyumba kufanikisha malengo ya elimu na sasa shule zinafunguliwa rasmi kuanzia tarehe 15 mwezi huu wa Januari na kurejesha nuru kwa wazazi hao ambao walikuwa wanasaidiana na walimu shuleni. Makala hii iliyoandaliwa na Assumpta Masso kutoka wavuti wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto , UNICEF, inafafanua zaidi. 

Audio Credit
FLORA NDUCHA/ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
3'31"
Photo Credit
© UNICEF/UNI342042/