Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana waendelea kushiriki katika utimizaji wa SDGs. Zauja Mohamed ni mmoja wao 

Vijana waendelea kushiriki katika utimizaji wa SDGs. Zauja Mohamed ni mmoja wao 

Pakua

Asasi ya Nuru Yetu Foundation chini ya uongozi wa msichana Zauja Mohamed ambaye alianzisha taasisi hii akiwa katika masomo yake ya sekondari miaka michache iliyopita, hivi karibuni imeandaa warsha kwa ajili ya wasichana. Warsha hii imewakutanisha wasichana na baadhi ya watu wenye ushawishi nchini Tanzania ili wasichana hao wapate miongozo mbalimbali ya kuwasaidia kupambana na changamoto za ndani ya jamii kama vile unyanyasaji wa kijinsia, kujikwamua kiuchumi, kielimu na kadhalika. Kupitia makala hii inayosimuliwa na Ahimidiwe Olotu wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa UNIC Dar es Salaam, Zauja Mohamed, anaeleza kuhusu warsha hiyo.  

Audio Credit
Anold Kayanda/Ahimidiwe Olotu
Audio Duration
3'39"
Photo Credit
UN SDGs