Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaeleza matukio ya wakimbizi na kuwatia moyo mwakani, Uganda

UNHCR yaeleza matukio ya wakimbizi na kuwatia moyo mwakani, Uganda

Pakua

Mwaka 2020 umekuwa wenye changamoto nyingi zilizoathiri watu wa tabaka mbalimbali ingawa kwa viwango tofauti.

Janga la COVID-19, mafuriko katika maeneo mbalimbali na halikadhalika janga la uvamizi wa nzige katika eneo la Pembe mwa Afrika na Afrika Mashariki yalivuruga maisha kiuchumi na kijamii.

Haya yote yamekuwa na madhara hasa kwa jamii zilizohatarini wakiwemo wakimbizi.

Uganda ni moja ya nchi zinazohifadhi wakimbizi wengi zaidi duniani ambako leo tunapiga darubini yetu kuangazia hali ilivyokuwa mnamo mwaka huu wa 2020 na ni matumaini gani yaliopo kwa mkimbizi na mhudumu w akibinadamu.

Basi Ungana na John Kibego aliyezungmuza na Rocco Nuri, Afisa Mkongwe wa Mawasiliaino katika shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini Uganda.

Audio Credit
Anold Kayanda/John Kibego
Audio Duration
3'47"
Photo Credit
UNICEF/Jimmy Adriko