Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Doris Mollel Foundation.

Mtoto kuzaliwa njiti si mkosi, akipatiwa matunzo anakua- Doris Mollel

Kila mwaka takribani watoto milioni 15 wanazaliwa njiti, yaani ujauzito ukiwa haujatimiza wiki 37. Takwimu hizo ni kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO ambalo linasema kuwa idadi inaongezeka. Kuzaliwa njiti ni moja ya sababu ya vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 na leo katika kuadhimisha siku ya kuhamasisha umma kuhusu watoto njiti, wito unatolewa ili kusaidia zaidi watoto hao. Taasisi ya Doris Mollel nchini Tanzania imejikita katika kusaidia watoto njiti kwa kuzingatia kuwa Mkurugenzi Mtendaji mwenyewe Doris alizaliwa njiti akiwa na uzito wa gramu 900.

Sauti
5'28"
UN News/ John Kibego

Wanahabari wahaha kutetea mazingira licha ya changamoto

Uhifadhi wa mazingira ni miongoni mwa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) ikiwa ni nguzo ya kudhibiti madhara ya mabadiliko ya tabianchi ambalo linachagiza mataifa kutunza na kukuza utunzaji wa mazingira.

Lakini kutokana na ukweli kwamba mazingira yanahifadhi rasilimali zinazotakiwa kutekeleza maendeleo, vuta nikuvute imeshuhudiwa kwenye nchi nyingi juu ya rasilimali za misitu na mali nyingine katika maeneo nyeti ikmazingira.

Sauti
2'54"
UN News/ John Kibego

Mikopo ya bodaboda yageuka kaa la moto kutokana na COVID-19 Uganda

Nchini Uganda, serikali ilipatia vijana mikopo ili kuwawezesha kujinasua kiuchumi na hivyo kuwa sehemu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Hata hivyo mafuriko katika Ziwa Albert na mlipuko wa ugonjwa wa Corona, COVID-19 vimevuruga uwezo wa vijana kurejesha mkopo huo. Sasa vijana kupitia vyongozi wao wanaomba serikali kutotumia mkono wa sheria dhidi ya wanaopata matatizo kuzingiatia ratiba ya ulipaji wa fedha walizopatiwa. Viongozi wa kisiasa wanaunga mkono ombi la vijana la kuelewa hali yao lakini wataalamu wa maendeleo ya  jamii wanasema, pesa hizo ni lazima zilipwe.

Sauti
3'40"
UNIC Tanzania/Ahimidiwe Olotu

Baba yangu asingemruhusu mama kusoma, nani angalikuwa anamlea hivi sasa? - Getrude

Suala la usawa wa jinsia ni suala mtambuka ambalo linahusisha taasisi mbalimbali ili liweze kufanikiwa katika taifa lolote lile. Hata hivyo taasisi ya familia ndio msingi mkuu wa kujenga au kubomoa dhana hii ambayo ni muhimu katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Nchini Tanzania, msichana Getrude ni shuhuda wa jinsi familia yake imekuwa msingi imara wa kutekeleza kwa vitendo usawa wa jinsia na sasa ameona matunda na kuamua kutumia uzoefu wake kunusuru watoto wa kike na wasichana ili wasitumbukie kwenye mtego wa kuwaengua na manufaa ya usawa wa jinsia. Je ni kwa vipi?

Sauti
5'7"
UN News/ John Kibego

Wanawake wachangia kwenye uhifadhi wa mazingira, Uganda

Uchafuzi wa mazingira huwagusa zaidi wanawake katika jamii nyingi hasa kwa kushikilia majukumu ya kitamaduni yakiwemo kilimo, upatikanaji wa kuni na hata dawa za asili kwa watoto wanapougua wakati huduma za kitaalamu ni ghali kupata au umbali wa kuzifikia.

Lakini kwa bahati mbaya huwa ni nadra wanawake wa vijijini kushirikishw akwenye mijadala ya mazingira. Hata hivyo nchini Uganda juhudi za asasi za kiraia kuunda vyama vya wanawake wanaohifadhi mazingira vinaleta nuru.

Sauti
4'4"
© UNHCR/Rocco Nuri

Mashahiri yatumika kupinga ukatili kwa watoto miongoni mwa wakimbizi Uganda wakati wa COVID-19  

Kufuatia mlipuko wa COVID-19 mnamo Machi mwaka huu nchini Uganda, shule zilifungwa na hivyo kuwaweka hatarini watoto kukumbana na ukatili wa kijinsia hasa katika makazi ya wakimbizi ambako huduma nyingi huwa hazitoshelezi jamii hizo. Kwa mantiki hiyo, shirika la Umoja wa Mataifa kupitia wadau wake wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali kuhamasisha jamii kuhakikisha ulinzi wa watoto wa kike na wale wa kiume. Sasa, watoto wenyewe wanashirikishwa katika kampeni ya kuwalinda kwa kuwapatia nafasi ya kuzungumzia changamoto na mikakati ya kuzikabili. 

Sauti
3'29"
UN Photo/Manuel Elías

Tunawapa vijana nafasi ya kuelewa mfumo mzima wa kazoi kabla hawajaingia rasmi-YUNA Tanzania

Ulimwengu uko katika muongo wa kuelekea utimizaji wa malengo 17 ya maendeleo endelevu. Lengo namba 8 linaongelea kazi bora au zenye hadhi pampja na ukuaji wa uchumi. Lengo hilo ni vigumu kulifikia iwapo hakuna maandalizi ya kutosha kwa wale wanaoandaliwa kufanya kazi na hivyo hali hiyo itasababisha sehemu ya pili yaani ukuaji wa uchumi nayo kutokufikiwa. Kwa msingi huo, ndipo asasi ya Umoja wa Mataifa ya vijana, YUNA Tanzania imeamua kuendesha mradi wa kuwapa nafasi vijana waliohitimu masomo na hata walioko masomoni bado ili wapate mafunzo kwa vitendo. 

Sauti
3'43"
UNCDF

Hatua zachukuliwa kudhibiti athari za COVID-19 kwa wanawake, Uganda

Mlipuko wa COVID-19 tangu ulipoanza umesambaratisha matumaini ya wengi kiuchumi na kijamii kutokana na vikwazo vya usafiri na biashara nyingi zikipigwa marufuku kama njia ya kudhibiti mlipuko huo. Wanawake na wasichana wameathirika zaidi kutokana na hali yao ya uhaba wa rasilimali hali ambayo pia imechochochea vurugu za nyumbani na ukatili wa kijinsia kwa mujibu wa ripoti za serikali mbalimbali.

Sauti
3'44"
© UNICEF/Schermbrucker

Muhimu ni kuwaambia watu sababu ya kwa nini unawaambia wapande miti-Dr Kalua

Nchi nyingi duniani hususan za afrika zinakumbwa na changamoto kubwa za kutunza mazingira. Mara nyingi hili hutokana na watu kutohamasishwa vya kutosha kuhusu manufaa yatokanayo ya utunzaji wa mazingira. Wakfu wa Green Africa ulioanzishwa mwaka 2000 umekuwa kwenye mstari wa mbele kuhakikisha kuwa watu wamepata kuelewa umuhimu wa utunzaji mazingira Barani Afrika na hata wameanzisha mradi ufahamikao kama 'Plant your age' yaani panda miti idadi sawa na umri wako. Mwandishi wa Kenya Jason Nyakundi amezungumza na muasisi wa wakfu huo wa Green Africa Dr Isaac Kalua.
Sauti
5'33"