Watoto wanasemaje kuhusu mkataba wa kimataifa wa haki za watoto?
Ikiwa leo ulimwengu unaadhimisha siku ya kimataifa ya mtoto, makala ya Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa inajikita mkoani Morogoro nchini Tanzania ambako watoto wanatoa maoni yao kuhusu siku yao hii na pia mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto, CRC, ambao umetimiza miaka 30 tangu ulipopitishwa.
Siku ya mtoto duniani ilianzishwa mwaka 1954 na huadhimishwa tarehe 20 mwezi Novemba ya kila mwaka ili kusongesha utangamano na ustawi wa kimataifa miongoni mwa watoto wote duniani.