Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wanasemaje kuhusu mkataba wa kimataifa wa haki za watoto?

Watoto wanasemaje kuhusu mkataba wa kimataifa wa haki za watoto?

Pakua

Ikiwa leo ulimwengu unaadhimisha siku ya kimataifa ya mtoto,  makala ya Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa inajikita mkoani Morogoro nchini Tanzania ambako watoto wanatoa maoni yao kuhusu siku yao hii na pia mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto, CRC,  ambao umetimiza miaka 30 tangu ulipopitishwa.

Siku ya mtoto duniani ilianzishwa mwaka 1954 na huadhimishwa tarehe 20 mwezi Novemba ya kila mwaka ili kusongesha utangamano na ustawi wa kimataifa miongoni mwa watoto wote duniani.

Ili kuyasikia maoni ya watoto basi kuhusu siku hii, haki zao na kile wanachokiona mashinani, ungana basi na John Kabambala kutoka redio washirika Tanzania Kids Time FM akizungumza na watoto hao kutoka katika shule mbalimbali za mkoa wa Morogoro.

Audio Credit
Brenda Mbaitsa/John Kabambala
Audio Duration
3'13"
Photo Credit
UNICEF