Mtazamo wa wazee kwa ndoa za utotoni huko Turkana

5 Novemba 2019

Ndoa za mapema ni jinamizi lililojikita mizizi katika tamaduni mbalimbali hasa zile za wafugaji barani Afrika, zikiathiri vibaya ustawi wa watoto wa kike. Jamii hizo ni pamoja na Karamajong Kaskazini Mashairki mwa Uganda, Toposa wa Kusini mashariki mwa Sudani Kusini nan a Masai na Turkana nchini Kenya.

Katika jamii ya Turkana Kenya, ndoa hizo ni sehemu ya utamaduni wao na unaathiri vibaya ustawi wa watoto wa kike kama vile kushindwa kupata elimu na hata madhara kwenye afya ya uzazi pindi wanapobeba ujauzito katika umri mdogo.

Ili kufahamu kwa undani kuhusu miendendo ya ndoa hizo, ungana na mwandishi wetu John Kibego katika sehemu ya pili ya makala ambapo anazungmuza na Mwenyekiti wa baraza la Wazee wa Kiturkana la Sub-kaunti ya Turkana South ambapo mzee huyo anaanza kwa kuelezea mtazamo halisi wa wazee.

Audio Credit:
Brenda Mbaitsa/John Kibego
Audio Duration:
3'57"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud