Ndoto yangu imetimia, nitajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu- Mtoto Rehema
Hatimaye mtoto Rehema Paul ambaye aliponea chupuchupu kuajiriwa kazi za ndani baada ya mwajiri wake kubaini kuwa umri wake haukuwa unaruhusu kufanya kazi, sasa ameanza masomo katika shule ya msingi Mchikichini, kwenye manispaa ya Morogoro nchini Tanzania. Mwajiri huyo, Herieth Mkaanga amefurahi sana kwani amefanikisha lengo namba 4 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs la kutaka elimu kwa watoto bila ubaguzi wowote ule na wakati huo huo kufanikisha ndoto ya mtoto Rehema ya kupata elimu.