Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Picha: UNHCR/M. Sibiloni

Ajira kwa vijana ndio mustakabali wa taifa

Ukosefu  wa ajira kwa vijana hususan kusini mwa jangwa la Sahara ni  kizingiti kikubwa kwa maendeleo

ya mataifa mengi barani Afrika kwasababu kundi hilo ndiyo nguvu kazi ya kila taifa.

Umoja wa Mataifa kupitia lengo nambari 8 la maendeleo endelevu SDGs, linalosema “ajira kwa wote na ukuaji wa uchumi”

unaendelea kuhimiza serikali na asasi za kiraia kuwawezesha vijana kujikwamua na umaskini kupitia miradi mbalimbali.

Sauti
3'41"
Cyril Villemain/UNEP

“Kenya tumepiga hatua katika nishati mbalala kuliko wakati wowote ule tangu uhuru” - Elmi

Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na  asasi mbalimbali za kiaraia, pamoja na serikali wamekuwa mstari wa mbele kutekeleza ahadi ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030.

Lengo nambari 7 ni moja kati ya malengo ya  maendeleo endelevu SDGs, yanayotoa fursa kwa serikali , na mahirika ya Umoja wa Maitaifa  kuwawezesha wananchi kupata nishati mbadala kwa bei nafuu lengo likiwa kuwakomboa lakini pia kulinda mazingira. 

Sauti
3'5"
UN/Eskinder Debebe

Mdundiko na ukatili vyahitaji vinamnyima haki msichana Kisarawe Tanzania:Jokate

Utamaduni ni kitu kizuri kinachoostahili kuenziwa lakini si kila utamaduni unapaswa kuendelezwa kwani tamaduni zingine zinamkandamiza mwanamke na mtoto wa kike kote duniani.

Kauli hiyo imetolewa na Jokate Mwegelo mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani nchini Tanzania. Katika wilaya hiyo bado utamaduni wa kuwacheza ngoma watoto wa kike maarufu kama (mdundiko) pindi wanapovunja ungo au kuwa vigori kuashiria wamepevuka na wako tayari kuolewa na hata kuwa mama, umekita mizizi na huwafanya wasichana wengi kutotimiza ndoto zao, kuzaa mapema na kukabiliwa na ndoa za totoni.

Sauti
3'44"
UN /Rick Bajornas

Najitahidi kuongea na barbaru ili waepuke vishawishi na kutimiza ndoto-Bi. Maina

Mimba za utotoni ni moja ya changamoto zinazokabili barubaru katika jamii nyingi duniani ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA linasema kila siku katika nchi zinazoendela wasichana barubaru walio chini ya umri wa miaka 18 hujifungua, hii ikiwa ni sawa na watoto milioni 7.3 wanaozaliwa kila siku. Na iwapo mimba zote zikijumuishwa idadi ya mimba za utotoni itakuwa juu zaidi.

Sauti
4'33"
UN News Kiswahili/ Grece Kaneiya

Dini ina mchango mkubwa katika ukombozi wa mwanamke Rwanda:Mchungaji Mwakasungura

Dini kama ilivyo na uwezo wa kuwaleta watu pamoja vivyo hivyo ina uwezo wa kumkomboa mwanamke sio Rwanda tu bali duniani kote. Kauli hiyo imetolewa na mchungaji Veronica Mwakasungura kutoka Rwanda anayehudhuria kikao cha kimataifa cha kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW63 kinachoendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York nchini Marekani.

Sauti
4'17"
Warren Bright/UNFPA Tanzania

Miundombinu ya kisheria imesaidia kumnasua mwanamke na mtoto wa kike Tanzania- Dkt. Jingu

Mkutano wa 63 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW ukiendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, wajumbe kutoka nchi mbalimbali wanajinasibu na kile ambacho wanafanya kuimarisha usawa wa jinsia na kumsongesha mwanamke na mtoto wa kike. Miongoni mwa wajumbe hao ni wale wa kutoka Tanzania na  hususan Dkt, John Jingu, ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto kuhusu miundombinu ya kisheria ambayo inatumiwa na nchi hiyo kuimarisha usawa wa jinsia.

Sauti
4'14"
CCBRT/Dieter telemans

Tanzania na mbinu bunifu za kuboresha huduma za afya kwa wanawake na watoto.

Ni mkutano ambao umewaleta pamoja takribani washiriki 9000 kutoka nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa. Kuanzia nchi za kipato cha juu, kati na cha chini ili kila mmoja apate kujifunza kutoka kwa mwingine. Na katika tukio lililoandaliwa na Tanzania kandoni mwa mkutano huo ndipo Dkt Ellen Mkondya Senkoro, Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi ya Benjamin Mkapa na Wakili Haika Harrison Ngowi wa shirika la Save the Children katika mahojiano haya na Arnold Kayanda  wameieleza UN News Kiswahili kile ambacho wamekuja kubadilishana na wenzao wa mataifa mengine. 

Sauti
5'40"
UNFPA/Ollivier Girard

Bila damu huna uhai, ndio maana nahamasisha uchangiaji wake Bungoma:Wengamati

Damu ni uhai na bila hiyo huna maisha ndio maana nikaamua kulivalia njuga suala la uchangishaji damu jimboni Bungoma. Kauli hiyo ni yake mke wa gavana wa jimbo la Bungoma nchini Kenya kama wanavyomuita mama wa Bungoma, Caroline Wesonga Wangamati.Maelfu ya kinamama duniani na hususan barani afrika hupoteza Maisha wakati wa kujifungua kwa sababu ya kutokwa na damu nyingi kabla na baada ya kujifungua. Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili kandoni mwa mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW63 unaoendelea kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani , Bi.

Sauti
4'24"
UN/Assumpta Massoi

Restless Development yazidi kuchagiza jamii kuhusu madhara ya ukatili wa jinsia

Ukatili wa jinsia ni suala ambalo limekuwa kikwazo kwa  maendeleo ya jamii hasa kwenye maeneo ambako mfumo dume umeshamiri na wanawake wanakumbwa na ukatili huo katika njia mbalimbali. Umoja wa Mataifa unatambua kuwa ukatili wa jinsia ni kikwazo na ndio maana unapigia chepuo usawa wa jinsi na kutokomeza mila potofu na hata sheria ambazo kwa njia moja au nyingine zinashamirisha ukatili wa jinsia. Hata hivyo changamoto ni pale ambapo jamii inakuwa ina uoga au hata pengine hawatambua kuwa kitendo fulani ni ukatili wa jinsia.

Sauti
3'46"