Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna kazi ya mwanaume wala mwanamke ni kujitosa tu:Njeri

Hakuna kazi ya mwanaume wala mwanamke ni kujitosa tu:Njeri

Pakua

Miriam Njeri mshona viatu mashuhuri hivi sasa nchini Kenya, anasema hakutarajia kuwa siku moja angekuja kuwa mshona viatu mkubwa na hata kumiliki kampuni, kazi ambayo kwa kawaida au kwa asililimia kubwa inaminiwa kuwa ya wanaume. Baada ya siku moja kutembelea kazi ya rafiki yake anayemiliki duka la kushona viatu aliamua naye kujitosa katika fani ya ushonaji viatu na kwa sasa amepata mafanio makubwa na kudhihirisha wito wa Umoja wa Mataifa wa kuwachagiza na kuwawezesha wanawake kwa kuwapa fursa . Mwandishi wa Nairobi  Jason Nyakundi amemtembelea kwenye karakana yake na kuzungumza naye kuhusu safari ya kuelekea kuwa fundi viatu.

Audio Credit
Jason Nyakundi/Miriam Njeri
Audio Duration
3'31"
Photo Credit
MINUSMA/Sylvain Liecht