Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kazi ya kinyozi yamwezesha mwanamke Nairobi Kenya kujiajiri na kutoa ajira kwa wengine

Kazi ya kinyozi yamwezesha mwanamke Nairobi Kenya kujiajiri na kutoa ajira kwa wengine

Pakua

Katika kufanikisha lengo namba tano la malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs ni muhimu pia kwa jamii kuondoa dhana ya kwamba kuna kazi za wanaume ambazo wanawake hawawezi kuzimudu. 

Kwa sass ni nadra sana upate mwanamke kinyozi lakini katika mtaa wa Kitengela ulio mjini Nairobi Lucy Muthoni amejitosa sawa  sawa katika hii fani ambayo kawaida huchukuliwa kuwa ya wanaume. Baada ya kuanzia kazi ya kuajiriwa kama mpokea wageni kwenye duka moja la kinyozi, kwa sasa yeye anamaliki duka la kinyozi. Mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi alimtembelea na kuzungumza naye.

Audio Credit
Brenda Mbaitsa/Jason Nyakundi
Audio Duration
4'1"
Photo Credit
UN Photo/Tobin Jones)