Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suala la afya lipo pia mkononi mwako kama mkenya-Waziri Kariuki

Suala la afya lipo pia mkononi mwako kama mkenya-Waziri Kariuki

Pakua

Hatua zimepigwa katika kuimarisha afya ya mamilioni ya watu, kuongeza umri wa kuishi, kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua na vita dhidi ya magonjwa yanayoambukiza. Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti ya utekelezaji wa lengo namba tatu la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs la  kuhakikisha afya kwa wote, hatua haziendi kwa kasi inayohitajika dhidi ya magonjwa makubwa kama vile malaria na kifua kikuu. Aidha karibu nusu ya watu wote duniani hawafikii huduma muhimu za afya huku wengi wakiteseka kutokana na ukosefu wa fedha. Umoja wa Mataifa unasema kwamba juhudi za pamoja zinahitajika kwa ajili ya kuhakikisha huduma ya afya kwa wote. Kenya kwa kuitikia wito huo imeanzisha mradi kwa ushirikiano na Shirika la afya ulimwenguni, WHO kuhakikisha huduma ya afya kwa wote. Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa au UN News Kiswahili alizungumza na Waziri wa Afya wa Kenya Sicily Kariuki miezi michache iliyopita kuhusu harakati hizo, mazungumzo ambayo Grace Kaneiya alifuatilia na kuandaa makala hii.

 

Audio Credit
Brenda Mbaitsa/Grace Kaneiya
Audio Duration
4'10"
Photo Credit
UN News/Grece Kaneiya