Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UNnewskiswahili/Patrick Newman

Vituo vyetu vya msaada wa sheria huanzishwa kwa kuzingatia mahitaij yaliyopo- WLAC

Nchini Tanzania kituo cha msaada wa sheria kwa wanawake, WLAC kimekuwa msaada hasa kwenye maeneo ambako bado kuna changamoto kuhusu haki na sheria. WLAC ikiwa inatekeleza majukumu yake katika wilaya 23 za mikoa ya Tanzania inalenga makundi tofauti tofauti hususan wanawake ikiwa ni katika kutekeleza lengo namba 16 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu amani, haki na taasisi thabiti. Flora Nducha alizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa WLAC, Wakili Theodosia Muhulo-Nshala ili kuweza kufahamu ni misingi ipi huzingatiwa katika kuanzisha vituo hivyo?

Sauti
4'15"
Julius Mwelu/UN-Habitat

Kaunti ya Nairobi na harakati za kulinda mazingira

Mji wa Nairobi, nchini Kenya ni kati ya miji inayokua kwa kasi zaidi barani Afrika, lakini suala la mazingira limekuwa changamoto kubwa. Kuanzia uzoaji taka, mifumo ya maji taka na hata ubora wa hewa ni baadhi ya changamoto zinazokumba mji huu. Idadi ya watu inazidi kuongezeka kila kukicha lakini miundo mbinu ya mazingira ni ile ile ya miaka nenda miaka rudi.

Sauti
4'31"
IOM/Amanda Nero

Uchafuzi wa Mto Kafu na athari zake wamulikwa, Uganda

Maeneo oevu ni sehemu muhimu katika suala zima la uhifadhi wa mazingira ambalo linapigiwa chepuo katika Malengo ya maendeleo endelevu (SDGS) hususani lengo namba 15, linalohimiza uhifadhi wa mazingira yakiwemo maeneo oevu  pamoja na matumizi endelevu ya misitu na kuzuia kuenea kwa hali ya jangwa.

Sauti
4'30"
FAO/Giulio Napolitano

Vijana kukamatwa juu ya mkopo wa serikali, Uganda

Katika harakati za kuhakikisha kwamba vijana wanapata ajira sio tu kwa kuajiriwa lakini kwa pia kwa kujiajiri kupitia ubunifu wa biashara mbali mbali, serikali zimeanza kuchukua hatua na kuweka programmu ambazo zinatoa mikopo kwa vijana kwa mfano vikundi kwa ajili ya kufanya biashara.

Lakini kuna changamoto mbali mbali ambazo bado zinakwamisha vijana katika ubunifu huo na kufanya biashara ambazo zinazaa matunda.

Sauti
4'9"
Picha ya UNAMID/ Hamid Abdulsalam

Wanawake wataka nafasi katika vyombo vya habari ili kustawi, Uganda

Nafasi ya mwanamke iwe katika siasa, uchumi au masuala mengine ya kijamii ni muhimu sana sio tu kwa kumuinua na kumuwezesha mwanamke lakini pia katika kuendeleza jamii kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Hivi sasa ajenda ya maendeleo endelevu au SDGs  ya mwaka 2030, inapigia chepuo uwezeshaji wa wanawake katika kila njia kupitia lengo namba 5. Na nchi mbalimbali zimeanza kuitikia wito huo japo bado kuna baadhi ya nchi mwanamke hana sauti na mchango wake hauthamininiwi.

Sauti
3'58"
UN News/ Anton Uspensky

Hatua zachukuliwa ili rasilimali kwenye Bahari Kuu zinufaishe mataifa yote

Rasilimali za baharini hususan zile zilizopo kwenye eneo lililo nje ya ukanda mahsusi wa kiuchumi au Exclusive Economic Zone, EEZ zimekuwa chanzo cha mvutano mkubwa si tu baina ya mataifa bali baina ya mataifa yenye nguvu kiuchumi na yasiyo na nguvu kiuchumi. Hii ni kwa kuzingatia kuwa mkataba wa sasa uliopo kuhusu rasilimali za baharí iwe samaki, matumbawe au chochote kile kipatikanacho baharini unagusia rasilimali zilizo nje ya eneo hilo la EEZ.

Sauti
4'26"