Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umuhimu wa nyuki kwa mazingira na kipato wangaziwa, Uganda

Umuhimu wa nyuki kwa mazingira na kipato wangaziwa, Uganda

Pakua

Nyuki wana mchango mkubwa katika maisha ya binadamu na mazingira na hasa umaarufu wake wa kuzalisha chakula kisichooza ambacho ni asali. Lakini manufaa ya nyuki yanaenda mbali zaidi ya asali hadi kwneye uzalishaji wa vyakula mbalimbali vya kawadia , dawa na pia utunzaji wa mazingira kwani nyuki ni sehemu muhimu ya ukuaji uendelevu wa mimea. Lakini sasa wadudu hao wako hatarini kutokana na  uchafuzi na uharibifu wa misitu na mazingira kwa ujumla ambayo ni maskani yao, yakiripotiwa kuwa changamoto duniani kote.

Katika kufuatilia suala hilo Mwandishi wetu wa Uganda John Kibego ameandaa makala hii iliyobeba onyo na mawaidha kuhusu uhsusiano kati ya nyuki na mazingira akizungumza na afisa msitaafu wa ufugaji wa nyuki wilayani Hoima, Bwana. Daudi Mugisa.

(Makala ya John Kibego)

Soundcloud
Audio Credit
Brenda Mbaitsa/ John Kibego
Audio Duration
3'49"
Photo Credit
FAO