Hofu yatanda juu ya uchafuzi wa Msitu Bugoma, Uganda
Kwa mujibu wa shirika la mpango wa mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP misitu ni rasilimali adhimu katika suala zima la uhifadhi wa mazingira na kudhibiti mabadiliko ya tabianchi. Pia hua ni msingi wa maisha na kipato kwa kuwezesha kilimo na upatikanaji wa nishati kwa asilimia kubwa ya watu dunaini hasa wale waishiyo katika maeneo ya vijijini. Matumizi endelevu ya rasilimali asili kwa maslahi ya mazingira limeaorodheshwa katika malengoya maendeleo endelevu au SDGs.