Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa UN na Tanzania wapeleka furaha kwa wanakijiji wa Magunga mkoani Tanga

Mradi wa UN na Tanzania wapeleka furaha kwa wanakijiji wa Magunga mkoani Tanga

Pakua

Mwezi  uliopita wa Oktoba, wakazi wa kijiji cha Magunda, wilaya  ya Korogwe mkoani Tanga nchini Tanzania waligubikwa na furaha isiyo kifani baada ya kushuhudia mashamba yao yakigeuka kuwa kitegauchumi na mtaji kwa ajili ya kuboresha maisha yao. Hii ni baada ya Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la mpango wa maendeleo UNDP na mfuko wa mazingira duniani, GEF na serikali yenyewe ya Tanzania kufanikisha mradi wa kugawa hati 250 za kumiliki ardhi. Mpango huu unalenga kufanikisha si tu matumizi bora ya ardhi bali pia kutokomeza umaskini ambalo ni lengo namba moja la malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Je nini kilifanyika? tuanze  basi na afisa wa UNDP Getrude Lyatuu na kisha mnufaika akihojiwa na Sawiche Wamunza, mkuu wa mawasiliano UNDP Tanzania.

 

Soundcloud
Audio Credit
Brenda Mbaitsa/ Sawiche Wamunza
Audio Duration
4'16"
Photo Credit
UN/Sawiche Wamunza