Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana tutumie fursa ili kufanikisha azimio la Cairo kuhudu idadi ya watu na maendeleo- Restless Development

Vijana tutumie fursa ili kufanikisha azimio la Cairo kuhudu idadi ya watu na maendeleo- Restless Development

Pakua

Mwaka 1994 huko mjini Cairo Misri kulifanyika mkutano wa kimataifa kuhusu idadi ya watu na maendeleo, ICPD ambao uliibuka na azimio lenye mambo makuu manne, ambayo ni elimu kwa wote ifikapo mwaka 2015, kupunguza vifo vya watoto wachanga na watoto, kupunguza vifo vya wajawazito na kuhakikisha kuwa huduma za afya ya uzazi ikiwemo uzazi wa mpango zinapatikana kwa watu wote ikiwemo vijana wa kike na wa kiume. Ni kwa mantiki hiyo miaka 25 baadaye mkutano  unafanyika Nairobi, Kenya kutathmini kile kilichofanyika na miongoni mwa washiriki ni vijana kutoka shirika la kiraia la Restless Development nchini Tanzania. Vijana hao wanawakilishwa na mwenzao ambaye amezungumza na mwandishi wetu wa Nairobi, Kenya Jason Nyakundi ili kuweza kufahamu mtazamo wao na matarajio yao baada ya mkutano huu wa siku tatu unaomalizika tarehe 14 Novemba 2019. Kijana anaanza kwa kujitambulisha.

Audio Credit
Brenda Mbaitsa/Jason Nyakundi
Audio Duration
3'52"
Photo Credit
UNFPA