Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usawa wa kijinsia si mwanamke kumkalia mwanaume bali kuweka uwiano wa maelewano kwa maslahi ya familia na jamii

Usawa wa kijinsia si mwanamke kumkalia mwanaume bali kuweka uwiano wa maelewano kwa maslahi ya familia na jamii

Pakua

Siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake zikiwa zimefikia ukingoni wiki hii, tumekwenda mkoani Geita nchini Tanzania ambako asasi ya kiraia ya Women's Promotion Centre inaendesha harakati za kupigania utu na haki za msingi za wanawake katika maeneo ya kanda ya ziwa nchini humo. Asasi hiyo inalenga kufanikisha uelewa na heshima kwa haki na utu wa wanawake ili waweze kuwa na jamii inayosimamia usawa wa jinsia. Adelina Ukugani wa redio washirika Storm FM amemhoji Afisa wa asasi hiyo Wakili Walta Carlos kuhusu jinsi wanavyosaidia kuwainua wanawake kwenye ukanda huo ambako yadaiwa jamii ina shaka na shuku juu ya wanawake kushika hatamu za uongozi.

Audio Credit
Adelina Ukungani
Audio Duration
6'2"
Photo Credit
UNICEF/UNI212587/Tremeau