Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

NEMA Kenya kwa kutambua athari za uchafuzi wa hali ya hewa imechukua hatua

NEMA Kenya kwa kutambua athari za uchafuzi wa hali ya hewa imechukua hatua

Pakua

Uchafuzi wa hewa unasababishwa na chemichemi haribifu ambazo zinasambaa hewani na athari zake ni mbaya kwani husababisha vifo vya mapema kutokana na magonjwa kama ya moyo, saratani pamoja na magonjwa ya matatizo ya kupumua.

Kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni uchafuzi wa hewa ulisababisha vifo milioni 7 kimataifa mwaka 2016. Huku vifo vingi vikitokea katika nchi zinazoendelea ambako sheria ni dhaifu au hazitekelezwi, uchafuzi wa hewa na magari yanayochagua mazingira havifuatiliwi.

Nairobi Kenya ni mfano wa mji ambao unakabiliwa na changamoto kubwa ya uchafuzi wa hewa kutokana na sababu mbalimbali na ni kwa kutambua hilo ndipo serikali imejizatiti kukabiliana na changamoto hiyo.

Basi ungana na Grace Kaneiya katika mahojiano na Evans Nyabuto mkurugenzi wa mawasiliano, mamlaka ya kitaifa ya kusimamia mazingira, NEMA ambaye anafafanua kile ambacho serikali inafanya kuzuia uchafuzi wa hewa hususan unaochangiwa na magari ya umma.

Audio Credit
Brenda Mbaitsa/ Grace Kaneiya/ Evans Nyabuto
Audio Duration
4'10"
Photo Credit
UN Environment/Jack Kavanagh