Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kituo cha televisheni cha lugha ya ishara ni habari njema kwa watu wanoishi na ulemavu Kenya

Kituo cha televisheni cha lugha ya ishara ni habari njema kwa watu wanoishi na ulemavu Kenya

Pakua

Malengo ya maendeleo endelevu SDGs yamewekewa ukomo wa kutekelezwa ambao ni mwaka 2030. Umoja wa Mataifa unataka kila mtu ashiriki ipasavyo ili asiachwe nyuma. Na ili kufikia hatua hiyo ni muhimu kila mmoja kwa nafasi yake ashiriki katika kumuinua mtu mwingine. Nchini Kenya, kijana Luke Kizito Ojambo Muleka ambaye kwa ubunifu wake amefanikiwa kuanzisha kituo cha runinga cha lugha ya alama au ishara kwa jina Signs TV ambacho huwadumia watu wenye ulemavu wa kila aina. Akiwa mdogo, Muleka, alishuhudia jinsi dada yake ambaye alikuwa kiziwi alivyopata changamoto kuelewa vipindi vya kawaida vya runinga vya sauti na picha na hivyo hilo likamsukuma kuanzisha kituo hicho.  Mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi alimtembelea na kuzungumza naye.

Audio Credit
Brenda Mbaitsa/ Jason Nyakundi
Audio Duration
4'1"
Photo Credit
Centre/Stéphanie Coutrix