Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ingawa tumevunjwa moyo hatujakata tamaa na mabadiliko ya tabianchi:Fazal

Ingawa tumevunjwa moyo hatujakata tamaa na mabadiliko ya tabianchi:Fazal

Pakua

Kutoafikiana kwa mataifa yanayochangia kiasi kikubwa cha hewa ukaa kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabianchi au COP25 uliohitimishwa mwishoni mwa wiki, kumezifadhaisha nchi zinazoendelea ikiwemo bara la Afrika ambalo si mchangiaji mkubwa wa hewa ukaa lakini ni muathirika mkubwa wa athari zake. Changamoto ilikuwa ni ibara ya 6 inayojikita na biashara ya hewa ukaa. Katika makala hii Flora Nducha anazungumza na Fazal Issa mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya kumbukumbu ya Sokoine nchini Tanzania na pia mratibu wa makundi tisa yaliyo chini ya shirika la Umoja wa Matifa la mazingira UNEP. Alishiriki mkutano huo na anafafanua kwanza kuhusu kipengele hicho cha ibara ya sita ya mkataba wa Paris

Audio Credit
Brenda Mbaitsa/ Flora Nducha/ Fazal Issa
Audio Duration
4'10"
Photo Credit
UN News