Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nachukuliwa kama adui katika jamii kwa sababu ya kazi ya kupinga ukeketaji Kajiado-Bi. Parit

Nachukuliwa kama adui katika jamii kwa sababu ya kazi ya kupinga ukeketaji Kajiado-Bi. Parit

Pakua

Suala la ukeketaji na ndoa za mapema ni baadhi ya changamoto zinazomkwamisha mtoto wa kike katika kufikia uwezo wake, lakini utokomezaji wa vitendo hivyo unakabiliwa na changamoto kwani vinachukuliwa kama sehemu ya utamaduni wa baadhi ya jamii.

Moja ya jamii hizo ni ile ya Maasai nchini Kenya ambapo licha ya kwamba kampeni na elimu inatolewa kutokomeza vitendo hivyo lakini bado vita hiyo haijafaulu. Kulikoni? Grace Kaneiya amezungumza na Dorcus Parit mwanzilishi na mkurugenzi wa  kituo cha mpito cha Hope Beyond huko kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambaye amemuelezea kazi za kituo hicho ambacho ni kimbilio kwa wasichana wanaoingizwa kwenye ndoa za utotoni au wale wanaokabiliwa na hatari ya kukeketwa.

Audio Credit
Brenda Mbaitsa/ Grace Kaneiya/ Dorcus Parit
Sauti
3'50"
Photo Credit
UNnewskiswahili/Patrick Newman